Na Avila
kakingo,Globu ya jamii.
KAMPUNI ya
Solution BLOCKS ikishirikiana na kampuni ya Anglo Gold Ashanti waandaa mkutano
wa Alhamisi ya kila mwezi ili kushirikisha taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za
kiserikali kuzungumzia kuchangia katika maendeleo katika jamii.
Hayo
yamesemwa na Makamo wa Rais wa Sustainability Aglo Gold Ashanti, Simon Shayo
katika ufunguzi wa mkutano ambao umejulikana kwa jina la THURSDAY TALK uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana.
Nae Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks (Facilitator), amesema kuwa Makampuni na
taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali lazima ziwajibike na kuelemisha
jamii pia na kutoa fursa kwa wadau wa maendeleo hapa nchini ili kushiriki vyema
katika kuleta maendeleo.
Pia ametoa
wito kwa makampuni, NGO, taasisi za Serikali pamoja na Asasi za kiraia kuwajibika
kushiriki vyema katika kuleta maendeleo
ya elimu,Afya,mazingira, maji pamoja na utawala bora katika taasisi hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana.
Makamu
wa Raisi-Sustainability Anglo Gold Ashanti-Mgodi wa Geita,, Simon Shayo
akizungumza na wadau waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika
hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na mgodi wa
dhahabu wa Geita jinsi unavyofanya kazi zake na kulinda afya za wananchi
wa maeneo hayo ili wasidhurike na uchimbaji wa madini hayo.
Afisa
Uhusiano na Mawasiliano wa Anglo Gold Ashanti -Mgodi wa Geita, Tenga
.M. Tenga akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya
Colosseum jijini Dar es Salaam jana ulioandaliwa na kampuni ya Solution
Blocks.
Baadhi
ya wadau waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya
Colosseum jijini Dar es Salaam jana kampuni ya Solution Blocks.
Kutoka
kushoto ni Makamu wa Rais-Sustainability Anglo Gold Ashanti, Simon
Shayo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna na
Afisa uhusiano na mawasiliano wa Anglo Gold Ashanti -Mgodi wa Geita,
Tenga .M. Tenga.
Kutoka
kushoto ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Anglo Gold Ashanti -Mgodi
wa Geita, Tenga .M. Tenga, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution
Blocks, Msomisi Mbenna na Afisa mahusiano na mawasiliano wa Benjamini
Mkapa HIV/AIDS Foundation, Deogratius Rimoy wakiwa katika picha ya
pamoja katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar
es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment