Wednesday, September 25, 2013

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA MONMOUTH HUKO NEW JERSEY-MAREKANI

Na Anna Nkinda
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekiomba chuo kikuu cha Monmouth cha mjini New Jersey nchini Marekani kufundisha wanafunzi wake lugha ya Kiswahili kama lugha ya kigeni ili wakazi wa eneo hilo waweze kuitumia katika mawasiliano pale itakapohitajika. 
 Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ametoa ombi hilo leo wakati akiongea na uongozi wa chuo hicho alipowatembelea yeye na ujumbe wake. 
 Alisema hivi sasa lugha ya kiswahili inakuwa kwa kasi na kutumika katika maeneo mengi hasa nchi za Afrika Mashariki na Kati hivyo basi nao wawafundishe wanafunzi wao ili wakienda katika nchi hizo iwe ni rahisi kwao kuwasiliana. 
 “Kiswahili ni lugha ya taifa letu la Tanzania ambayo tunaitumia katika mawasiliano, mkiwafundisha wanafunzi wenu lugha hii nao watawafundisha wenzao hivyo itakuwa ni rahisi kwao kuwasiliana hasa wakisafiri na kukutana na watu wanaotumia lugha hii”, alisema Mama Kikwete. 
 Kwa upande wake makamu rais wa chuo hicho Dk. Edward Christensen alimshukuru mama Kikwete kwa kutembelea chuo hicho na kusema kuwa ombi lake la chuo hicho kufundisha lugha ya Kiswahili wamelisikia na wataangalia jinsi gani watalifanyia kazi.
 Aidha Dk. Christensen aliwaomba wakufunzi na watu wenye utaalamu wa mambo mbalimbali kutoka nchini Tanzania kwenda katika chuo hicho kufanya midahalo na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho. 
 Chuo hicho kinawanafunzi wapatao 6300 kutoka ndani na n je ya nchi 29 na kinatoa kozi mbalimbali zikiwemo za Sayansi na sanaa katika ngazi ya cheti, shahada na shahada ya uzamili.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth kilichoko huko New Jersey nchini Marekani mara tu baada ya kuwasili chuoni hapo tarehe 24.9.2013. Mama Salma yupo nchini Marekani akifuatana na Rais Jakaya Kikwete anayehudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa unaofanyika New York.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Chuo Kikuu cha Monmouth baada ya kuwasili chuoni hapo. Kulia kwa Mama ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi akifuatiwa na Naibu Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ramadhani Mwinyi, na Ms Janet Mahoney,wa Chuo Kikuu cha Monmouth na kushoto kwa Mama Salma ni Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu hicho, Bwana Saliba Sarsar, Makamu Rais wa Chuo cha Monmouth anayeshughulikia mahusiano ya kimataifa na Mwisho ni Bwana John McLaughlin, kutoka Shirika la Footprints for Education International la nchini Marekani.
 Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth Dr. Paul Brown,akimtembeza Mama Salma Kikwete maeneo mbalimbali ya chuo hicho. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth baada ya Mama Salma kumkabidhi Jarida litolewalo na Taasisi ya WAMA .
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kitabu kutoka kwa Dkt. Edward Christensen, Vice President for Information Management. Chuo Kikuu hicho kilitoa zaidi ya vitabu  4000 kwa ajili ya Tanzania. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni pamoja na Waziri wa Afya Dr. Hussein Mwinyi na Makamu Rais wa Chuo Bwana Sarsar na Mwishi ni nBwana John McLaughlin.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anazungumza na Bwana Kevin Williams, Mwalimu kutoka shule ya Asbury Park. Shule hiyo ina uhusiano na shule ya sekondari ya WAMA, iliyoko huko Nakayama, wilayani Rufiji, mkoani Pwani. Katikati ni katibu wa WAMA Bw. Daudi Nasibu. 
Picha zote na John Lukuwi

No comments:

Post a Comment