Wednesday, September 25, 2013

Rais Kikwete azindua Mpango wa Kuzishirikisha Sekta mbalimbali kupambana na Malaria


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya kuzindua rasmi Mpango mpya wa Kimataifa utakaohusisha Sekta mbalimbali katika kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria duniani. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani chini ya uratibu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Taasisi ya Roll Back malaria Partbership.
iongoni mwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo akiwemo Waziri wa Afya na Ustawai wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi (Mb.) (kulia) wakimsikiliza Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.
Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando Guebuza akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa kuzishirikisha Sekta mbalimbali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.                                           


Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Guebuza wakiwa na wageni waalikwa wengine.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula akiwa na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mpango wa kukabiliana na malaria kwa kuzishirikisha sekta mbalimbali.

Mshauri wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Milenia, Prof. Jeffrey Sachs akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo.
Mwakilishi wa Taasisi ya Roll Back Malaria Partnership mjini New York Bw. Herve Verhoosel akimkabidhi Mhe. Rais Kikwete mfano wa kifaa cha kufukuzia mbu  wakati wa uzinduzi wa mpango wa mapambano dhidi ya malaria.

Mhe. Mwinyi akifurahia jambo na Bi. Rebeca Grynspan kutoka UNDP pamoja na Bi. Ellen Maduhu, Afisa kutoka Ubalozi wa Tanzania, New York.
Picha na Rosemary Malale

No comments:

Post a Comment