Monday, June 20, 2011

MAKAZI YA WATU YANAPOGEUZWA KUWA MACHIMBO YA MCHANGA

Ankal,


Inashangaza sana kuona sehemu iliyopimwa Viwanja na ni makazi ya watu na kuna barabara za mitaa ZILIZOGHARIMU FEDHA NYINGI  za umma halafu wanajitokeza watu wachache wasiopenda MAENDELEO wanakuja KUCHIMBA mchanga na wanapoambiwa na wakazi wa eneo hili husika kwamba ondokeni watu hawa bado wanaendelea kuchimba mchanga na wala hawaogopi.

Iko hatari kubwa sana ya kuharibiwa eneo la MIVUMONI block 5 lililoko wilaya ya KINONDONI, kuna vijana wameanza kuchimba eneo lililo karibu kabisa na Transforma ya Block 5 barabara ya LAGOS ambayo ilitugharimu sana kuipata . Na zaidi sana eneo wanalochimba mchanga ni for PUBLIC use na ambalo WANANCHI wa eneo hili tunapaswa kulilinda.

Wananchi wa eneo hili tumeshafanya juhudi nyingi sana kuwafukuza lakini bado wanaendelea kuchimba. Tulipowauliza kwa nini wanachimba mchanga kwenye eneo hili ambalo ni Residential area, Wanasema na kutuuliza bila aibu kwa nini tunawazuia kufanya kazi yao?

Wananchi wa eneo hili tuliweza kuwasilisha taarifa hizi kwa ofisi ya serikali ya Mtaa wa Mivumoni , kwa DC wa Kinondoni pamoja na Municipal Director wa Kinondoni lakini bado jamaa hawa wanaochimba mchanga wanakuja usiku na malori na wanachimba na wanaendelea kuharibu mazingira. Mpaka Sasa inaonyesha hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa maana watu hawa wanaochimba mchanga bado wanaendelea licjha ya sisi wananchi wa eneo hili kutoa namba za magari yanayohusika kuchimba na kubeba mchanga katika eneo hili.

Kinachoumiza zaidi ya kuwa na HANDAKI ambalo halita weza kuzibwa leo wala kesho kutwa litakuwa ni gharama sana kwa sisi wakaazi wa eneo hili kulifukia na ni hatari zaidi pale mvua kubwa zitakapoendelea kunyesha maana inaweza kusababisha mmomonyoko mkubwa sana wa ardhi katika eneo hili.

Sio handaki tu cha kushangaza zaidi ni kwamba wanaikaribia TRANSFORMA iliyoigharimu TANESCO fedha/gharama kubwa sana  kuipata na kuja kuiweka katika eneo letu la Mivumoni.

Angalieni picha (zilizoambatanishwa hapa) jinsi zinavyoonyesha eneo hili linavyoharibiwa. Ni  wakati muafaka sasa kwa vyombo husika kuchuka hatua kuzuia uharibifu huu mkubwa wa mazingira kwani si MUDA MREFU uliopita tangu kuadhimisha siku ya MAZINGIRA duniani.

Inashangaza kuona watu hawa wanaochimba mchanga wanaendelea KUCHIMBA MCHANGA na  kuzidi kuharibu MAZINGIRA ya eneo hili. Sisi WANANCHI wa Mivumoni tunatoa tena TAARIFA hii kwa wote wanaohusika KUCHUKUA HATUA KALI kuzuia uharibifu huu

Asante
Sisi Wananchi wa Mivumoni na wapenda MAZINGIRA

No comments:

Post a Comment