Monday, October 1, 2018

KITUO CHA SANAA CHA URUSI NA TANZANIA WAMKUMBUKA ALIYEKUWA MCHORAJI NGULI MSAGULA

Na Agness Francis,globu ya Jamii

Kituo cha utamaduni cha Urusi na Tanzania wanaadhimisha wiki ya kumbu kumbu ya aliyekuwa mchoraji nguli hapa nchini Boniface Msagula.

Msagula aliyezaliwa 1939 kijiji cha ndanda wilayani masasi mkoa wa Lindi na kufariki 2005 anakumbukwa na kituo hicho kwa kuonyesha sanaa ya michoro yake ya aina ya tinga tinga alichora enzi ya uhai wake.

Akizungunza jijini Dar es Salaam aliyekuwa Mkurugenzi wa kituo hicho Rifat Pateev amesema maonesho hayo yameana jana katika hicho na kilele chake itakuwa Oktoba 6 mwaka huu.Amefafanua muda wa kuanza kwa maonesho hayo ni saa nne asubuhi na kumalizika saa 10 jioni na hakuna kiingilio,na watu waliokuwa wakijishuhulisha na Sanaa hapa jijini Dar es Salaam hasa Rifat Pateev aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha utamaduni cha Urusi na Tanzania. 

Akifafanua zaidi Rifat alisema alivutiwa Sana na viwango na uasili wa kazi za Sanaa za Msagula."Miongoni mwa wasanii wa kitanzania ambao nimezishuhudia kazi zao ni Damian Msagula ana michoro ya kipekee,rangi katika michoro na picha zake zilikuwa zikiendana vizuri na kwa uhakika,hiki kilikuwa ni kipaji muhimu kwake"amesema Rifat Pateev. 

Pia ametaja baadhi ya Maonyesho ya picha michoro na Sanaa aliyowahi kufanya Msagula katika sehemu mbali mbali ni mwaka 1976 New Africa hotel Dar es salaam, mwaka 1992 Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, mwaka 1993 Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, mwaka 1995 Telelom building Bonn, mwaka 1996 Dunia ya mizimu ya Msagula kituo cha utamaduni cha urusi na Dar es Salaam.Pia mwaka 1998 simulizi za Msagula kituo cha utamaduni cha urusi na Dar es Salaam,mwaka 1999 Tinga tinga na 2000 Msagula-Solo Exhibition. 

Akimzungumzia Mchoraji huyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Elias Jengo amesema Msagula akiwa na miaka 15 kabla ya kuanza kufanya kazi ya sanaa yake ya kuchora alikuwa mwanamuziki na kuanzisha bendi kadhaa.Amezitaja bendi hizo ni Uhuru Jazz,The black hammer boxing na Skylarks.Pia ilipofika mwaka 1972 alijishughulisha na uuzaji wa matunda kutoka mkoani Tanga kwenye eneo la duka la Morogoro Stores ambapo ndio alikutana na wasanii wa michoro ya Tinga tinga.

Profesa Jengo amesema msanii huyo ambaye hakuwahi kuwa na familia wala kuwa na watoto alikuwa na urafiki wa muda mrefu na watu waliokuwa wakijishughulisha na sanaa katika Jiji la Dar es Salaam hasa Rifat Pateev aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Urusi na Tanzania.

No comments:

Post a Comment