Diwani wa kata ya Baraki Mh Mwita Laurian akikabidhi vyeti kwa wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Erengo ambapo mahafari hayo yameambatana na harambee kwa lengo la kuboresha vyumba vya madarasa hayo.
Na Frankius Cleophace, Rorya.
Wadau wa elimu Wilayan Rorya Mkoni mara wametakiwa kuendelea kuchangia fedha kwa lengo la kuboresha Vyumba vya madarasa katika shule za msingi wilayani Rorya Mkoani Mara ili kuweza kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia ikiwemo shule ya Msingi Erengo ambayo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo pamoja na upungufu wa Madarasa.
Wadau wa elimu Wilayan Rorya Mkoni mara wametakiwa kuendelea kuchangia fedha kwa lengo la kuboresha Vyumba vya madarasa katika shule za msingi wilayani Rorya Mkoani Mara ili kuweza kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia ikiwemo shule ya Msingi Erengo ambayo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo pamoja na upungufu wa Madarasa.
Wananchi kwa kuliona hilo katika mahafari ya darasa la saba Shule ya Msingi Erengo wanachangi fedha kupitia harambee ambapo wamechangia zaidi ya Millioni moja pamoja na vifaa vyenye thamani ya shilingi Millioni moja huku wakiomba serikali kuwaunga mkono ili kuendeleza jitihada hizo , Makutano Gijagida ni Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Erengo na Charles Maganya ni mratibu Elimu kata ya Baraki wanazungumzia changamoto za shule hiyo huku wakipingeza nguvu za wananchi haowaliojitoa kuchagia katika harambee iliyoandaliwa.
Wanafunzi wa darasa la saba awakitoa burudani ya nyimbo katika mahafari hayo.
Maganya amesema kuwa shule yake inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa vyumba vya madarasa hivyi amezidi kuomba wadau wa elimu na wazazi kuzidi kujitoa kwa wingi kwa lengo la kutatu changamoto hiyo.
“Mazuingira ya shule yakiwa mazuri wanafunzi watapenda kusoma pia walimu watkaa shuleni hivyo sasa wazazi na wadau wa elimu kwa mkoa wa Mara na nje ya mkoa tuendelee kujitoa” alisema Mwalimu mkuu.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Baraki Mh Mwita Laurian anasema kuwa shule ya Msingi Erengo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uchakavu wa majengo hivyo amesema kuwa kama diwani wa kata hiyo atazidi kuhimiza wananchi kuendelea kujenga vyumba vya madarasa ili serikili iweze kumalizia huku akitafuta wadau mbalimbali wa elimu ili kutatua changamoto za shule hiyo.
Wananchi wa kijiji cha Baraki pamoja na wazazi wakiwa katika mahafari hayo.
Aidha Anipha Misapa ambaye ni afisa mtendaji wa kijiji cha Baraki anasema kuwa majengi yote yenye changamoto yanaenda kukarabaitiwa huku Mwenyekiti wa kijiji hicho Emmanuel Daud akizidi kusisitiza jamii kujitolea kwenye suala la Maendeleo hususani ujenzi wa Vyumba vya madarasa katika shue za msingi na Sekondari.
Wananchi wa kijiji cha Baraki wameamua kufanya harambee kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Erengo iliyopo wilayani Rorya mkoani Maraambapo wamepata vifaa vya ujenzi vyenye thamani zaidi ya shilingi Millioni moja pamoja na fedha zaidi ya million moja zilizochangwa na wanachgi na wadau wa elimu katika mahafari hayo huku wengine wakiutoa ahadi mbalimbali lengo ni kuboresha shule hiyo.
Ni vyumba vya madarasa vinavyotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Erengo iliyopo wilayani Rorya Mkoani Mara ambavyo siyo rafiki kwani vimechakaa sana.
No comments:
Post a Comment