Thursday, June 28, 2018

TPW YATOA SH MILIONI 40 KWA WANAWAKE 250 WILAYANI MONDULI KUFANIKISHA UFUGAJI WA NYUKI



Msimamizi wa miradi wa Asasi ya Watu na Wanyama ya (TPW), iliyopo Simanjiro mkoani Manyara akizungumza wakati wa kukabidhi mradi mpya wa uhifadhi mazingira na ufugaji nyuki kwa Baraza la Wanawake wa Kikufugaji Monduli (BAWAKIMO), Asasi hiyo imewapa Sh milioni 40 kama mtaji.
Mkurugenzi wa Baraza la Wanawake wa Kifugaji Monduli (BAWAKIMO), Mary Morindat akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uhifadhi mazingira na ufugaji nyuki kwa wanawake wa 250 kutoka Kata ya Lemooti na Mswakini wilayani humo.

Msimamizi wa miradi wa Asasi ya Watu na Wanyama ya (TPW), iliyopo Simanjiro mkoani Manyara akizungumza wakati wa kukabidhi mradi mpya wa uhifadhi mazingira na ufugaji nyuki kwa Baraza la Wanawake wa Kikufugaji Monduli (BAWAKIMO), Asasi hiyo imewapa Sh milioni 40 kama mtaji.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta akizungumza wakati wa ufunguzi wa mradi wa uhifadhi mazingira na ufugaji wa nyuki wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta akipokea mfano wa Hundi ya zaidi ya Sh milioni 40 kutoka kwa Msimamizi wa Miradi wa Asasi ya Watu na Wanyama (TPW),Revocatus Magayane kwa ajili ya mtaji wa mradi wa ufugaji nyuki kwa wanawake 250.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta akibadilishana mawazo na Msimamizi wa Miradi wa TPW Revocatus Magayane mara baada ya kukabidhi mradi wa ufugaji nyuki kwa wanawake 250 wa Kata ya Lemooti na Mswakini.
Mratibu wa Miradi kutoka BAWAKIMO Angela Kagashe akizungumza na baadhi ya wanawake wanachama wa baraza hilo juu ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo mpya wa uhifadhi mazingira na ufugaji wa nyuki wilayani Monduli.


Na Ripota Wetu, Arusha

MAISHA ya wanawake 250 waliopo Kata ya Lemooti na Mswakini Monduli mkoani Arusha yanataraji kubadilika baada ya Asasi ya Watu na wanyama(TPW) kuwapatia Sh.milioni 40 za mradi wa uhifadhi mazingira na ufugaji nyuki.

Kupitia mradi huo wanawake hao kutoka kwenye vijiji sita vya Mswakini Juu, Mswakini chini, Lengolwa, Lemooti, Oldonyo na Naitolia watapatiwa mizinga 475 itakayofungwa kwenye maeneo ya vikundi 25 vya watu 10. Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo leo, Msimamizi wa miradi Asasi ya TPW Revocatus Magayane amesema mradi huo wanautekeleza kwa ushirikiano na Baraza la Wanawake wa Kifugaji Monduli (BAWAKIMO).

Magayane amewataka wanawake hao kutoa taarifa za maendeleo ya mradi kila wakati hatua itakayowawezesha kuwa na mwanzo mzuri wa utekelezaji. Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta aliwataka wanawake hao kutoingiza siasa kwenye shughuli zinazohusiana na maendeleo kwani kufanya hivyo kutawafanya wakwame kufikia ndoto zao.

“Uchumi hauna itikadi ya kisiasa, mkiingiza siasa kwenye masuala haya mtahawanyika na kushindwa kufikia mnachokihitaji kama kuwa na maisha mazuri kusomesha watoto na kujenga nyumba bora na kisasa,” alisema Kimanta. Naye Katibu wa BAWAKIMO Nai Zakayo ameishukuru TPW kwa kuwawezesha kupata na kuanzisha mradi huo wa nyuki kwenye kata mbili za wilaya hiyo.

Aidha ameiomba TPW kuwafikia wanawake wengi zaidi kwani bado wanayo maeneo mengi katika Kata nyingine ambazo zinaweza kufanya miradi ya uhifadhi wa mazingira na ufugaji wa nyuki.

No comments:

Post a Comment