Tuesday, June 5, 2018

Halotel yazindua laini mpya za watu mashuhuri (VIP).


-Ni laini zenye gharama nafuu Zaidi, hazihitaji kujiunga kifurushi

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imezindua laini mpya za watu mashuhuri zilizopewa jina la VIP zitakazo wawezesha wateja wa mtandao huo kufanya mawasiliano kwa makato ya gharama nafuu zaidi kwa kila dakika na MB za intaneti watakazo tumia.

Laini hizo za VIP zitawawezesha wateja wa mtandao wa Halotel nchi nzima kuweza kupiga simu au kutumia intanenti kwa gharama nafuu kwa kutumia salio la muda wa kawaida wa maongezi bila kuwa na ulazima wa kujiunga na kifurushi chochote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Mhina Semwenda, amesema kuwa, uzinduzi huo wa laini za VIP ni mwendelezo wa ubunifu na maboresho ya huduma za mawasiliano kwa wateja wa Halotel kwa kuwaokolea muda na gharama ambapo badala ya mteja kutumia muda na gharama kujiunga na vifurushi vya kupiga simu kwa mtandao wa Halotel na mitandao yote au vifurushi vya intaneti mteja ataweza kutumia salio la muda wa maongezi kupiga simu au kutumia intaneti bila kuhofia matumizi makubwa ya makato kwa gharama nafuu zaidi.

“Huduma hii inawalenga wateja wa vipato vya aina zote, wale wenye matumizi ya kati, na matumizi makubwa, ambapo katika laini hii ya VIP makundi hayo yamegawanywa kwa kupewa majina ambayo ni Silver kwa wateja wenye matumizi madogo, Gold kwa wateja wa matumizi ya kati na Diamond kwa wateja wa matumizi makubwa. Makundi haya yana lengo la kukidhi mahitaji ya kila mteja kulingana na kundi alilomo.” Alisema Semwenda na kuongeza.

“Mfano kwa mteja atakayenunua laini ya VIP ya Silver yenye thamani ya shilingi elfu tano (5,000) kwa pesa hiyohiyo anaweza kupiga simu Halotel kwenda Halotel kwa gharama ya makato ya shilingi thelathini (30) tu kwa dakika ambapo kwa makato ya gharama ya kawaida ni shilingi (228) kwa dakika ambapo ni mara punguxo la mara saba(7) ya gharama za kawaida. 

Vile vile mteja katika kundi hili anaweza kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya makato ya shilingi arobaini na tano (45) tu kwa dakika tofauti na makato ya gharama ya kawaida ambayo ni shilingi (228) kwa dakika ambapo ni punguzo mara tano (5) ya gharama za kawada. Kwa MB 1 mteja atatumia intanenti kwa gharama ya shilingi nne (4) tu akiwa na laini ya Silver ya VIP gharama ambayo ni mara saba(7) pungufu ya makato ya gharama ya kawaida ya shilingi 30.72 kwa MB huku akifurahia kutumia Facebook bure.” Alisema Semwenda.

Mteja yeyote wa Halotel wa kawaida ana uhuru wa kuweza kubadili laini yake na kuwa laini ya VIP na kuweza kufurahia kupiga simu Halotel na mitandao yote pamoja nakutumia Mb za intanenti kwa kupiga *148*66# kisha anachagua namba tisa (9) na hivyo kuendelea kuchagua kundi atakalohitaji kujiunga, si hivyo tu mteja wa Halotel wa kawaida anaweza kuendelea kujiunga na vifurushi kama kawaida endapo atahitaji.

Hii ni moja ya maendeleo ya teknolojia katika kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wetu ambao wamekuwa na imani kubwa ya huduma zetu siku zote” alisema Tito.

“Tunatarajia huduma hii ya VIP itaongeza nafasi na uwezo wa mawasiliano kwa wateja wetu na kwa watanzania wote, na kuokoa kiasi kikubwa cha gharama za mawasiliano zinazokatwa wakiwemo wafanya biashara, wafanyakazi na wateja wengine walioko sekta zingine mijini na vijijini ambako maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kuwasiliana, biashara na kupata taarifa mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia intaneti kwa uhakika. Alihitimisha Semwenda.”
Meneja wa idara ya ushirika Halotel Emmanuel Tito Malyeta, Halotel akiwaeleza waandishi wa Habari, akitoa ufafanuzi mbele ya waandish wa Habari katika uzinduzi wa huduma ya VIP ambapo Mteja yeyote wa Halotel wa kawaida ana uhuru wa kuweza kubadili laini yake na kuwa laini ya VIP na kuweza kufurahia huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel akiwaeleza waandishi wa Habari, akitoa ufafanuzi mbele ya waandish wa Habari katika uzinduzi wa huduma ya VIP, ambayo ni mwendelezo wa ubunifu na maboresho ya huduma za mawasiliano kwa wateja wa Halotel kwa kuwaokolea muda na gharama katika matumizi yao ya kila siku. Kulia ni Meneja wa idara ya ushirika Halotel Emmanuel Tito Malyeta. 

No comments:

Post a Comment