Monday, May 7, 2018

Bei mpya za mafuta yatangazwa zanzibar

Na Mwashungi Tahir Maelezo 7-5-2018.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma, Nishati na Maji Zanzibar ZURA imetoa taarifa juu ya bei za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia kesho siku ya Jumanne ya tarehe 8-5-2018.

Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Maisara Kaimu Mkuu kitengo cha uhusiano Khuzaimat Bakar Kheir alisema ZURA ina kawaida ya kupanga bei kwa kuzingatia mambo yafuatayo.Alisema wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la Dunia (Platts Quatations ) katika mwezi wa Machi , 2018 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanya mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Mei ,2018.

Pia alisema gharama za uingizaji na uhifadhi wa Mafuta katika Bandari ya Dar es salaam pamoja na gharama za kuyasafirisha tena hadi Zanzibar .Vile vile gharama za Usafiri , Bima na ‘Premium ‘ hadi Zanzibar .Thamani ya shilingi ya Tanzania kwa Dola , kodi ya Serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejereja.Kaimu huyo alisema Bei za mafuta kwa mwezi Mei 2018 zimeshuka ikilinganishwa na bei za Mwezi wa April 2018 , sababu za kushuka kwa bei ni .

Kushuka wastani wa mwendo wa mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la Dunia (Platts Quatations ).Kushuka kwa Gharama za uingizaji na uhifadhi katika Bandari ya Dar es salaam pamoja na gharama za kuyasafirisha tena hadi Zanzibar , hasa “Demurrage charges ambapo mafuta ya Petrol yameshuka kwa Tsh . 5 kwa lita kutoka Tsh. 18.96 hadi Tsh 13.98,mafuta ya Dizeli yameshuka kwa Tsh. 6 kutoka Tsh 21.08 kwa lita hadi Tsh. 15.53 na mafuta ta Taa haijabadilika kwa mwezi wa Mei, 2018.

Kushuka kwa gharama za usafirishaji , Bima na faida ya muagizaji (Premium) ambapo mafuta ya Petrol yameshuka kwa Tsh . 49 sawa Asilimia 60% , mafuta ya Dizeli yameshuka kwa Tsh 8 sawa na Asilimia 20% na Jet A-1(mafuta ya taa) haijabadilika.

Khuzaimat aliendelea kusema Bei ya reja reja ya mafuta ya petrol kwa mwezi wa Mei, 2018 imeshuka kwa Tsh 89 kwa lita kutoka Tsh 2, 344 ya Mwezi wa April ,2018 hadi Tsh hadi Tsh 2, 255 kwa lita katika mwezi wa Mei , 2018 sawa na punguzo la Asilimia 3%.

Bei ya reja reja ya mafuta ya Dizeli kwa Mwezi wa Mei, 2018 imeshuka kwa Tsh. 64 kwa lita kutoka Tsh 2, 314 ya Mwezi wa April , 2018 hadi Tsh 2, 250 sawa na Asilimia 2%.Pia alisema bei ya reja reja mafuta ya taa kwa Mwezi wa Mei. 2018 haijabadilika ni Tsh 1.740 kwa lita.

Bei ya reja reja ya Mafuta ya Banka kwa Mwezi wa Mei , 2018 imeshuka kwa Tsh 78 kwa lita kutoka Tsh . 2,156 kwa lita katika Mwezi wa April, 2018 hadi Tsh, 2,078 katika mwezi wa Mei, 2018 sawa na punguzo la Asilimia 3%.

Na bei ya reja reja ya mafuta ya Ndege kwa Mwezi wa Mei imeshuka kwa Tsh 2.5 kwa lita kutoka Tsh. 1,812.63 kwa lita katika mwezi wa April , 2018 hadi Tsh 1,810.21 katika Mwezi wa Mei, 2018 sawa na asilimia 0.13%.
Kaimu Mkuu kitengo cha uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti waHuduma, Nishati na Maji Zanzibar( ZURA) Khuzaimat Bakar Kheir akizubgumza na waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya bei za mafuta Zanzibar (Picha na Kijakazi Abdalla -Maelezo Zanzibar.).

No comments:

Post a Comment