Thursday, March 1, 2018

Vanessa Mdee aungana na mastaa maarufu duniani wanaomiliki majukwaa ya mtandaoni


Vee Money App katika kilele cha maendeleo ya mziki Afrika na dunia nzima
Vanessa Mdee anaungana na mastaa maarufu duniani ambao wanamiliki ‘majukwaa ya mtandaoni’ ya kuwasiliana na mashabiki wao

Je unafahamu kitu gani kinachowafananisha Taylor Swift, Ciara, na Vanessa Mdee? Naam, pamoja na kwamba wote ni wasanii wenye sauti nzuri na vipaji vikubwa, wote watatu wanamiliki majukwaa ‘app’ za kuwasiliana na mashabiki wao mtandaoni.

Hii ni njia mpya inayotumiwa na wasanii wakubwa ambao wana mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii kama Facebook na Instagram, ukweli ni kwamba pamoja na mitandao hiyo mikubwa ya kijamii kutengeneza mabilioni ya dola kila mwaka wasanii hawapati mapato ya moja kwa moja kutokana na biashara hiyo.

Sababu nyingine kubwa ambayo inawafanya wasanii kama Kim Kardashian kuwa na majukwaa yao mtandaoni ‘app’ ni kwa sababu hawamiliki mashabiki wao wa mtandaoni ila mitandao ya kijamii ndiyo ina haki juu ya watu wanaoitumia, hii inamaanisha msanii mkubwa akifungiwa akaunti yake ya Facebook au Instagram anaweza kukosa njia ya kuwasiliana na mashabiki wake (Rob Kardashian ni mfano halisi).

Pamoja na ukweli kwamba majukwaa‘app’ pia zinaruhusu wasanii maarufu kuuza bidhaa mbalimbali na tiketi kwenye simu za mkononi lakini cha muhimu zaidi, inasaidia wasanii kufaidika kutokana na makampuni makubwa kutangaza kupitia majukwaa yao.

Kama ilivyonukuliwa kwenye mtandao maarufu wa FORBES, tangu Juni 2014 Kim Kardashian ameingiza mapato ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 200. Hiyo si pesa ndogo na ni hivyo ni rahisi kuwaelewa wasanii kama Taylor Swift, Ciara, na mwanadada anayeitikisa Afrika Mashariki, Vanessa Mdee ambao wote wamezindua majukwaa yao ili kukamata fursa hiyo katika mazingira ya sasa yaliyojaa maendeleo makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Vanessa Mdee amechukua fursa hii kwa kuzindua Vee Money App mwezi Januari mwaka huu. Vee Money App, ambayo ilitengenezwa na kampuni ya teknolojia ya Marekani ya Converge Media, imepokelewa na inaendelea kufanya vizuri kwenye soko.

Pamoja na kutoa maudhui ya kipekee kwa mashabiki wake, Vee Money App pia ni jukwaa kwa watangazaji ambao wanataka kuwafikia mashabiki halisi wa Vanessa. Hapo awali, makampuni walipotaka kutangaza bidhaa zao kwa mashabiki wa Vanessa waliingia mikataba moja kwa moja na Facebook au Instagram (ambao ndio wana taarifa za mashabiki) bila kumhusisha Vanessa mwenyewe. Uwepo wa Vee Money App unamfanya sasa Vanessa kuwa mstari wa mbele katika masuala yote yanayohusiana na matangazo kwa mashabiki wake hivyo watangazaji sasa wanaweza kuwasiliana na kuingia mikataba moja kwa moja na yeye binafsi.

Mdee bado hajaacha mitandao ya kijamii kama Instagram na Twitter, hata hivyo, maamuzi yake ya kuzindua jukwaa lake la kuwasiliana na mashabiki kwa njia ya mtandao ni jambo la ujasiri linalompa mwelekeo mzuri katika sekta ya mziki kama inavyoonekana kwa Taylor Swift na Ciara. Kwa Mdee ‘Vee Money App’ ni maendeleo ya asili katika ukuaji wake kwa ujumla katika sekta ya mziki.

‘Kwa kadri ninavyoendelea kuwa katika mziki nimetambua kwamba umiliki wa kazi zako ni muhimu sana; kuanzia kumiliki mziki wako, mashabiki wako, na majukwaa yako ya mtandaoni na kama hutafanya hivyo mtu mwingine atakusaidia’ alisema Mdee.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa Converge Media, Nick Brunelle, umiliki wa wasanii ndio sababu ya uwepo wa kampuni hiyo. "Tulitaka kujenga mazingira ambapo wasanii kama Vanessa wanaweza kuwa na umiliki si tu katika mapato ya matangazo lakini pia umiliki katika taarifa na habari zinazohusiana na majukwaa yao" alisema Brunelle.

Maana yake ni kwamba tofauti na majukwaa mengine ya mitandao ya kijamii, Vanessa anamiliki habari zote zinazozalishwa na Vee Money App na ana udhibiti wa taarifa hizo na namna zinavyotumiwa. "Vanessa hakika ameyapokea mabadiliko mapema hasa kwa Afrika," aliongeza. "Ameona wazi mziki unapoelekea kimataifa na yeye amefuata mkondo huo na kuwa kinara barani Afrika"

Kwa sasa jukwaa la Vanessa Mdee, Vee Money App, inapatikana bure kupitia ‘Apple App store’ na ‘Google play store’ (Kama vile kwa Taylor Swift na Ciara apps) . Wakati utaamua namna wasanii wanaomiliki majukwaa yao watavyokuwa wamepiga hatua huko mbeleni lakini kwa hakika kuna ongezeko kubwa la mashabiki wanaotamani kuwa karibu zaidi na wasanii wanaopenda kuliko ilivyo sasa katika mitandao ya kijamii. Na Mdee ameamua kuwa kinara katika kutimiza kiu ya mashabiki wake.

No comments:

Post a Comment