Thursday, March 1, 2018

KUJISAJILI WCF LENGO NI KUMUONDOLEA MZIGO WA GHARAMA MWAJIRI,KULINDA HAKI ZA MFANYAKAZI: MAVUNDE




NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOSHI

SERIKALI ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuhakikisha wafanyakazi wanalindwa na kupata haki zao pindi wanapopatwa na madhara yatokanayo na kazi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amesema mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro..

Mheshimiwa Mavunde ameyasema hayo jana (Machi 1, 2018), wakati akiendelea na ziara yake ya kushtukiza ili kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria linalowataka waajiri wote katika sekta rasmi,(umma na binafsi), waliopo Tanzania Bara kujisajili na kuchangia kwenye Mfuko huo.

Kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Ikiwa Mwajiri hatajisajili kwenye Mfuko, atakuwa ametenda kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi na akipatikana na hatia adhabu yake ni kulipa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000,000 (Milioni Hamsini) au kifungo kisichozidi miaka mitano jela au adhabu zote kwa pamoja, alisema Mhe. Mavunde.

Mheshimiwa Mavunde ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anslem Peter na Kaimu Kamishna kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, alibaini Mkoa wa Kilimanjaro wenye jumla ya Waajiri 1,039 ni waajiri 525 tu ndio wamejisajili huku wengine 514 bado hawajajisajili na Mfuko.

“Serikali ilikwishatoa matamko mbalimbali yanayowahimiza waajiri kutekeleza takwa hilo la kisheria, na leo hii hakuna njia nyingine, Waajiri hawa tuliowabaini hapa Mkoani Kilimanjaro naagiza WCF iwapeleke mahakamani haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake.” Alisema.

Baadhi ya waajiri ambao Naibu Waziri na timu yake walifanya ukiaguzi huo ni pamoja na kampuni ya Machare Investments, Scholastica Schools iliyoko Himo nje kidogo ya mji wa Moshi.Alisema sio lengo la serikali kuwatisha au kuwadhalilisha waajiri hao bali nia ni kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa lakini pia kuwaondolea jukumu waajiri la kuwahudumia wafanyakazi wao wanapopatwa na madhara wakiwa kazini.

“Tunataka ninyi wawekezaji, (waajiri), mjielekeze kwenye shughuli zenu za msingi kwa maana ya kufanya uwekezaji na biashara zenu na hili la kumuhudumia mfanyakazi aliyepatwa na madhara kazini lishughulikiwe na serikali.” Alisisitiza.

Tayari Mhe. Mavunde amefanya ziara kama hiyo mkoani Mwanza na Shinyanga na kubainisha kuwa operesheni hiyo ya kuwabaini waajiri wasiotekeleza takwa hilo la kisheria litafanyika nchi nzima, na kuwataka waajiri kufanya hivyo haraka ili wasijikute kwenye matatizo.

“Tumewasambaza maafisa wetu wa WCF mikoani na wanaednelea na utaratibu wa kuwafuikisha mahakamani waajiri wote ambao wameshindwa kufuata sheria.
Naibu Waziri ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akiongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anslem Peter, (kulia) na Mhasibu wa Shule ya Scolastica, Bw.Moshi W.Moshi, wakati wa ziara yake ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi, (WCF) ambapo ilibainika shule hiyo kubwa mjini Moshi haijatekeleza takwa hilo la kisheria 
Mhaisbu wa Shule ya Scolastica mjini Moshi, Kilimanjaro Bw. Moshi W. Moshi, na Mkuu wa shule hiyo Bw.Michael Shiloli, wakisikilzia maagizo ya Naibu Waziri Mvunde. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, (kulia), akijadili jambo na Kaimu Afisa Kazi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi.Neema Msyalika na Afsia Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bw. Sebere Fulgance.
Mhe. Mavunde akizungumza na Mkurugenzi wa Machare Investments, (kulia)
Bw. Anselim Peter akizungujza na waandishi wa habari
Mhe. Mavunde akisisitiza jambo kwa viongozi wa shule ya Scolastica.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, (kulia), akijadili jambo na Kamishna wa kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, (katikati), na Kaimu Afisa Kazi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi.Neema Msyalika

No comments:

Post a Comment