Friday, March 23, 2018

KIKAO CHA RAIS MAGUFULI,WAFANYABISHARA KIWE CHACHU YA MAENDELEO KATIKA NCHINI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KWA Ujinga wangu naomba niseme mapema tu, mimi si mfanyabiashara ila 
nimekuwa karibu kwasababu nanunua bidhaa za wafanyabishara.

Nanunua bidhaa za wafanyabishara kulingana na mahitaji yangu ya kila 
siku.Ndio ukweli maana maisha yangu ni kwamba nikijipata vijesenti naenda dukani nanunua nachojitaji.Kwa kuwa nimekuwa karibu na wafanyabishara , nikiri nimekiwa nikifuatilia 

mambo yao mbalimbali.Hata wanapotoa malalamiko yao kuhusu kukwamishwa kwa mambo yao nimekuwa nikisia.Malalamiko ya tozo kubwa za kodi kwenye masuala ya biashara nayo nimekuwa nikiwasikia wafanyabishara wakilalamika.

Nawasikia kwasababu mbali ya kuwa ni sehemu ya mteja wao , bado nami ni Mtanzania ambaye nashukuru Mungu ni muumini wa kufuatilia kila jambo nchini kwetu.Hata Rais wangu Dk.John Magufuli wakati unatoa maagizo kwa Waziri wa Fedha na Mpango kukaa na Mamalaka ya Mapato Tanzania(TRA)kuangalia namna ya tozo za kodi.

Ukasema kuwa kodi zimekuwa kubwa kiasi cha kufanya kuwa kero.Ukaeleza 
namna ambavyo unataka kodi iwe jambo la heshima kwa Taifa na si kuwa kero kwa mlipaji.Kwa Ujinga Wangu baada ya kusikia utakutana na wafanyabishara kutoka maeneo mbalimbali nchini.Nikasema kwenye mazungumzo hayo lazima kitaeleweka.

Rais Magufuli ukaamua kutoa nafasi ya kila mfanyabishara kutoa dukuduku lake.Nakumbuka kwenye mkutano huo ambao wewe uliongoza ulieleza namna ambavyo unataka kumsikia kila mmoja wao.Wafanyabishara nao kwa kuwa kuna mambo ambayo yalishikuwa kero kwao waliamua kusema kila kitu.Hakuna ambacho wamekificha maana waliona ndio sehemu pekee ya wao kusikilizwa.

Wakaeleza changamoto ambazo wanakutana nazo kutoka kwa TRA.Wakaeleza namna ambavyo wanaojihusisha na biashara ya mazao kuharibikia njiani.Wakaeleza namna ambavyo wanatamani Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya biashara.Wafanyabishara hao wakaelezea mambo mengi.Wakaeleza namna ambavyo wanaamini kikao hicho kati yao na Rais kitakuwa na mafanikio makubwa.Kama nilivyotangulia kueleza awali mimi si mfanyabiashara lakini nimevutiwa na mazungumzo kati ya pande hizo mbili.

Kw Ujinga wangu nikawa nawaza kwanini kikao hichi kimechelewa kufanyika?Hata hivyo nikajijibu mwenyewe kuwa ratiba yako imebana kutokana na majukumu mbalimbali ya kuwatumikia Watanzania.Kwa mtazamo wangu kikao hicho kitakuwa chachu ya maendeleo ya nchi yetu.Tunatambua mchango wa wafanyabishara katika kujenga uchumi wa nchi yetu.

Natambua TRA kutokana na makadirio ya kodi kuwa juu , kuna wafanyabishara wengi wamefunga maduka yao.Wameyafunga si kwasababu wanapenda bali mazingira ya kodi yamekuwa kikwazo kwao.Nieleze ni kweli kuna malimbikizo ya madeni ya kodi ambayo wafanyabishara wanadaiwa lakini nilidhani TAR wangekuwa na jukumu la kukaa na wafanyabishara na kisha kuangalia njia nzuri ya kuhakikisha madeni yanalipwa na wafanyabishara wanaendelea kufanyabishara.

Naamini kikao kati ya Rais Magufuli na wafanyabishara kitafungua ukurasa mpya katika sekta ya biashara nchini.Rais wakati anazungumza kwenye kikao hicho alitumia nafasi hiyo kushughulikia baadhi ya malalamiko.Akatumia nafasi hiyo kutoa maagizo na maelekezo kulingana na hoja za wafanyabiashara.

Hata hivyo kukosekana kwa baadhi ya mawaziri au makatibu wakuu kwenye kikao hicho kilisababisha Rais Magufuli kuhoji kwanini hawakufika.Sababu ya kuwaliza ilitokana na kuamini kuna baadhi ya mambo yanaweza kushughulikiwa na wizara moja kwa moja.

Pamoja na kukosekana kwa baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu ambao nao walialikwa kwenye kikao hicho bado lengo la mkutano ulifanikiwa.Hakika mkutano huo umefungua ukurasa mpya kati ya Rais Magufuli na wafanyabishara.Sote tunafahamu kuna wakati ilijengeka dhana kuwa hakuna uhusiano mzuri kati ya wafanyabiashara na Serikali.Hata hivyo unapomsikiliza Rais Magufuli na wafanyabishara hao unabaini hakuna tatizo bali yapo mambo yaliyokuwa yanasababisha manung'uniko.

Kabla ya kuhitishwa kwa kikao hicho, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipata nafasi ya kutoa maelezo yake na akatumia nafasi hiyo kuonesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya maofisa wa TRA kuwa kero katika eneo la ukusanyaji kodi.Akasema wamesababisha kufungwa kwa maduka bila sababu za msingi na akatumia nafasi hiyo kuelezea hatua ambazo amechukua kukomesha tabia hiyo.

Wakati Rais Magufuli wakati anahitimiza kikao hicho, amesema yapo baadhi ya mambo ufumbuzi wake utakuwa wa haraka na mengine watakwenda kujipanga ili kutafuta ufumbuzi wake.

Akawaambia wafanyabishara hao kuwa katika utawala wake watatajirika sana na anachokifanya ni kuondoa kona kona ambazo zimekuwa zikikwamisha wengine.Akaleza namna ambavyo baadhi ya wafanyabishara wanatozwa kodi kubwa na wengine hawatozwi kodi.

Akawahakikishia kuwa Serikali yake inawapenda wafanyabiashara na itakuwa nao bega kwa bega.Rais akasema katika eneo la uchumi kuna vita kubwa na hivyo ni Watanzania kwa umoja wao kusimama imara.Ni maoni yangu kuwa Rais Magufuli baada ya kikao hicho kuna mengi ambayo ameyapata kutoka kwa wafanyabishara hao na yakifanyiwa kazi tutasonga mbele.

Kwa Ujinga Wangu naomba nieleze wazi kikao hicho kimenifanya hata mimi nisiye mfanyabishara nianze kufikia kufanya biashara kwani mazingira ya biashara chini ya Rais yanayonekana kuanza kuwa bora zaidi.Ahsante kwa kunisoma
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  alipokuwa akiendesha  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam hivi karibuni 

No comments:

Post a Comment