Monday, October 30, 2017

WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA NA MAAFISA WA SERIKALI NA TASAF MJINI DSM.

 MMoja wa maafisa wa TASAF Bw. Hamis Kikwape (aliyeshika kipaza sauti) akiwasilisha taarifa baada ya kurejea kutoka Zanzibar na Morogoro akiwa na wadau wa maendeleo.
 Baadhi ya wadau wa maendeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF wakiwa katika kikao cha pamoja cha kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.
 Mmoja wa maafisa wa TASAF Bi. Tumpe Lukonge (aliyeshika kipaza sauti) akiwasilisha taarifa ya ziara kwa wajumbe wa kikao kazi cha wadau wa maewndeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF ,kinachojadili utekelezaji wa  Mpango wa Kunusuru Kaya masikini.

Baadhi ya wadau wa maendeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF wakiwa katika kikao cha pamoja cha kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga (kulia) akiwa na Kiongozi wa Shughuli za TASAF katika benki ya Dunia Bw. Muderis Mohamed wakiwa katika kikao kazi hicho.



 

NA ESTOM SANGA-TASAF.

Wadau wa Maendeleo,Maafisa wa Serikali na Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF wanakutana jijini Dar es salaam baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.

Vikao kazi hivyo vilivyoanza kwenye makao makuu ya TASAF mjini Dar es salaam vitapitia taarifa zilizopatikana kwenye maeneo yaliyotembelewa na wadau hao wa maendeleo na maafisa wa serikali ili kuona Mafanikio na Changamoto za utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini unaohudumia takribani kaya milioni MOJA NA LAKI MOJA nchini kote.

Wakiwa katika maeneo hayo ya utekelezaji wajumbe walipata fursa ya kukutana na baadhi ya walengwa wa Mpango huo na kuona shuhuda mbalimbali za namna Mpango huo unavyoendelea kupunguza adha ya umasikini kwa kutumia fedha wanazozipata kuanzisha shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato.

Miongoni mwa miradi iliyoanzishwa na walengwa ni pamoja na ufugaji wa kuku wa kienyeji, mbuzi,nguruwe na hata ng’ombe wa maziwa na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba za matofali na kuezeka kwa mabati tofauti na hali waliyokuwa wakikabiliwa kabla ya kuingizwa kwenye shughuli za Mpango.

Vikao kazi hivyo vinavyoambatana na ziara kwenye maeneo ya Utekelezaji wa Mpango hufanywa kila baada ya miezi SITA kwa lengo la kuboresha huduma kwa walengwa na kusaidia nia ya serikali ya kujenga mazingira wezeshi kwa wananchi kukuza mapato yao kwa kuanzisha miradi midogo midogo kulingana na mazingira yao.

Mikoa ambayo wadau hao wa maendeleo na maafisa wa serikali na TASAF wametemebelea ni pamoja na Tabora, Kigoma, Njombe,Ruvuma,Kilimanjaro, Morogoro, na Zanzibar.Baada ya vikao hivyo taarifa ya maendeleo ya utekelezaji na mapendekezo yakayofikiwa itawasilishwa serikalini. 

No comments:

Post a Comment