Monday, October 30, 2017

DKT.FAUSTINE NDUGULILE AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA CHAMA CHA WATAALAMU WA MAGONJWA YA FIGO MJINI DODOMA

Naibu Waziri wa Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto dkt.Faustine Ndugulile akiongea kwenye mkutano huo wa wataalamu wa magonjwa ya figo nchini.Mkutano huo wa siku mbili unafanyika kwenye Hotel ya Morena Mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali nchini,Wadau wa Maendeleo pamoja na wataalamu wengine kutoka nchi za Kenya,Sudan,India pamoja na Norway
Makamu wa Rais wa Chama cha wataalamu wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT), Dkt.Paschal Ruggajjo akiongea dhima kubwa ya mkutano huo ni teknolojia ya upandikizaji wa viungo nchini ili kuweza kuhudumia wagonjwa takribani milioni 23.
Baadhi ya Wataalamu wa magonjwa ya figo waliohudhuria mkutano huo.Mkutano huo ni wa siku mbili ambapo watajadili dhana mbalimbali ya ugonjwa wa figo ikiwemo kutoa elimu kwa umma ili kuweza kukabiliana na magonjwa ya figo pamoja na upandikizaji.Tanzania imekua ikipeleka wastani wa wagonjwa thelathini na tano(35) kwa mwaka nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza figo na gharama ya kupandikiza nje ya nchi ikiwemo India ni shilingi milioni 75 hadi 77 kwa mtu mmoja ikiwemo kupandikiza,nauli pamoja na malazi
Makamu wa Rais wa cChama hicho akimpa zawadi mmoja wa wataalamu wa figo ambaye amefanya tafiti na kuwasilisha mada ya katika mkutano huo Profesa Ainory Gesase ambaye ni mkufunzi wa Chuo cha Sayansi ya Tiba.
Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi wa mkutano huo Dkt.Ndugulile akiwa na wataalamu wa figo nchini pamoja na wadau wengine wa ndani ya nchi na nje ya nchi.
Naibu Waziri akisalimiana na washiriki wa Mkutano huo mara baada ya ufunguzi.Dkt.Ndugulile alisema Serikali mgonjwa mmoja anahitaji wastani wa shilingi za kitanzania 37,620,504 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia gharama za kusafisha damu nchini
Mashine za kusafisha figo(Dialysis Machine) ambazo zimefungwa kwenye hospitali nchini.Serikali imefunga mashine katika hospitali nchini ikiwemo UDOM (10),Hospitali ya Muhimbili (42), Hospitali ya Rufaa Mbeya(5), Hospitali ya Rufaa Bugando (10), KCMC(10),Hospitali ya Misheni Serian(10),Hospitali ya NSK Arusha(5),TMK(10),Regency(15),Hurbert Kairuki(5), Aga Khan(10) na Access(10).Mashine hizo zina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 783 kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) na 391 kwa huduma ya malipo ya papo kwa papo


Picha zote na Wizara ya Afya

No comments:

Post a Comment