Monday, September 4, 2017

MFAHAMU JAPO KWA UCHACHE JAJI DAVID MARAGA -MSABATO MWENYE IMANI KALI

.....'I am a God fearing person who believes in, and endeavours to do, justice to all irrespective of their status in society.....' 

Mzaliwa wa Januari 12, 1951, Jaji wa Mahakama ya juu nchini Kenya, David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti na kuamuru kurudiwa ndani ya siku 60 zijazo. (Land Mark Case).

Wakenya na wadau wengine kwingineko duniani wamempongeza Jaji Maraga kwa kuwa jasiri kutengua uchaguzi wa mtu aliyemchagua rais Uhuru Kenyatta mbali na kurudisha imani katika idara huru ya mahakama.

Magazeti kadhaa ya Kenya yamemtaja jaji Maraga kuwa mtu wa maadili kutokana na hatua yake ya kuwa muumini shupavu wa kanisa la Seventh Day Adventist Church (SDA).

Aliripotiwa akiliambia jopo lililokuwa likimhoji kwamba iwapo atachaguliwa kuwa jaji mkuu nchini Kenya hatosimamia kesi siku ya Jumamosi , ambayo ni siku ya kupumzika kwa waumini wa kanisa hilo.

Wengine wamedai kwamba huenda hii ndio sababu kikao cha kwanza cha kesi ya kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta kilianza mwendo wa saa moja usiku siku ya Jumamosi baada ya siku ya Sabato kuisha........kama mna kumbukumbu hii pia iliwahi kutokea kwa Waziri mkuu wa zamani wa Israel Bwana Ariel Sharon ambaye aliondoka mkutanoni majira ya saa kumi na mbili baada ya sabato kuingia kuhu akimwacha Clinton kutoamini macho yake (Wayahudi na sabato huwaelezi kitu).........

Wafaransa pia hawatamsahau Benjamin Netanyahau kwani baada ya kuandaa itifaki zote za kumpokea walijikuta wakiambiwa kwamba hangeweza kwenda nchini humo Ijumaa jioni HADI SABATO ITAKAPOKWISHA ...........yaaani kesho yake jumamosi tena baada ya jua kuzama.
Imeripotiwa kuwa wakati alipokuwa akikaguliwa alikabiliwa na madai kwamba alikula hongo lakini yeye aliwashangaza wengi kwa kutangaza katika runinga za taifa akiapa kwa kushikilia kitabu kitukufu cha Biblia kwamba hajawahi kuchukua hongo katika maisha yake. Jaji Maraga alifuzu kama wakili miaka 40 iliyopita kutoka chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuhudumu kama wakili wa kujitegemea

Alichaguliwa Jaji 2003 na kujiunga na Mahakama ya Rufaa 2012. Ameoa na ana watoto watatu.
Jaji David Maraga alichukua mahala pake Jaji mkuu mstaafu Willy Mutunga ambaye muda wake wa kuhudumu ulikamilika 

Maraga mwenye umri wa miaka 66 sasa aliwashinda wenzake 13 ambao pia walituma maombi yao ya kugombea wadhfa huo wa juu, akiwemo Jaji wa Mahakama ya juu, Jacton Ojwang na Smokin Wanjala , msomi Makau Mutua miongoni mwa wengine. Majaji hustaafu wakiwa na umri wa miaka 70 hatua inayoaminisha kwamba Maraga atahudumu kwa miaka minne zaidi ijayo.

Hata hivyo mapema mwaka huu aliripotiwa kumkemea mtu aliyemchagua, Rais Uhuru Kenyatta.
Wakati akifanya kampeni nyumbani kwa Jaji Maraga, Rais Uhuru Kenyatta alinukuliwa akisema kuwa wakaazi wa eneo hilo wanafaa kumpigia kura kwa sababu alimpatia kazi ''mwana wao''.
Hata hivyo Jaji mkuu kupitia idara ya mahakama JSC alisema kuwa yeye sio MRADI WA SERIKALI.
Rais Uhuru Kenyatta hapo awali alikuwa amesema kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama, ijapo kuwa alihoji ni kwa nini watu sita wanaweza kutoa uamuzi unaokwenda kinyume na matakwa ya Wakenya.

 Hatahivyo baadaye Raisi Uhuru alisema kuwa Majaji hao walikuwa wamelipwa na ''watu wa kigeni pamoja na wajinga wengine''. 'Maraga na wahalifu wake wameamua kubatilisha uchaguzi. Sasa mimi sio tena Rais mteuliwa bali Rais aliye mamlakani. Maraga anapaswa kujua kwamba sasa mimi ni rais anayehudumu''

Licha ya vitisho hivyo, Rais hana uwezo wa kumfuta kazi jaji mkuu ambaye muhula wake mmoja unakamilika wakati atakapofikisha miaka 70 kwa mujibu wa Katiba ya Kenya ya 2010 
167. (1) A judge shall retire from office on attaining the age of seventy years, but may elect to retire at any time after attaining the age of sixty-five years.
(2) The removal of a judge may be initiated only by the Judicial Service Commission acting on its own motion, or on the petition of any person to the Judicial Service Commission.
kadhalika Jaji Mkuu David Maraga alijitokeza mnamo Jumanne, Mei 16, kukashifu uongozi wa National Super Alliance (NASA) kwa matamshi yao kuhusu IEBC na idara ya Mahakama. 

Hii ndiyo sababu Maraga anaonya upinzani dhidi ya kuingilia maswala yaliyo kortini. “Sitajibu matamshi ya kiholela kutoka kwa wanasiasa wakati wa kipindi cha kampeni. Nataka Wakenya wawe na imani na idara ya mahakama kama taasisi huru na isiyo na ubaguzi,” Maraga alisema.

No comments:

Post a Comment