Tuesday, August 29, 2017

RC TABORA ATAKA MAELEZO ALIYECHOMA MOTO KATIKA CHUO CHA ARDHI

Na Tiganya Vincent.

SERIKALI Mkoa wa Tabora imeagiza kutafutwa na kuchukiwa hatua kali na kupata maelezo ya watu waliohusika na uchomaji moto katika maeneo ya Chuo cha Ardhi Tabora na kusababisha uharibifu mkubwa wa mistu asili na miti iliyokuwa imepandwa katika eneo hilo kama hatua za uhifadhi wa mazingira.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri baada ya kukuta eneo la Chuo hicho likiwa limeungua na moto wakati wa ziara ya ya kukagua vitalu vya kuoteshea miti ikiwa ni maandilizi ya zoezi la upandaji wa miti.

Alisema kuwa haiwezekani wananchi wanajitoa kwa moyo kupanda miti katika kampeni inayoendelea kisha watu wachache wanaamua kuua miti na kuharibu mazingira.

Mwanri aliongeza kuwa inasikitisha kuona hata sehemu za Taasisi za umma kama hiyo zinaacha moto unaunguza miti na wakufunzi wapo, wanachuo wapo bila kuchukua hatua ya kuuzima na kuwasaka waliohusika.

Alisema kitendo kinaonyesha jinsi wao nao wanahusika kwa namna moja au nyingine katika kuchangia uharibifu ulifanyika katika Chuo chako.
Kufuatia kitecho hicho Mkuu wa Mkoa alimwagiza Afisa Mazingira wa Manispaa ya Tabora kwenda kwa Mkuu wa Chuo kupata maelezo nini kilitokea na hatua zilizochukuliwa kwa wahusika na kama hawachukua hatua kwa wahusika basi Sheria za Mazingira zichukue mkondo wake.

Aliongeza kuwa pamoja na hatua hiyo zitakazochuliwa aliagiza uongozi wa Chuo hicho kuhakikisha wanarudishia miti yote iliungua mapema iwezekanavyo.“Nimesikitishwa na kitengo nilichokiona katika eneo la Chuo cha kuchoma moto na kuunguza miti ,kiwa kwa watu wasomi ambao wanatakiwa wawe mfano wa utunzaji wa mazingira wao ndio wanakuwa wa kwanza kuharibu mazingira kwa kuchoma moto…nimesikitishwa sana” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Naye Afisa Mazingira wa Manispaa ya Tabora William Mpangala alisema hadi hivi sasa Ofisi yake imekwishakamata watu 27 kwa makosa ya uchomaji moto ovyo na kuwapiga faini ya kuanzia 50,000/-

Alisema kuwa viongozi wa Taasisi wafahamu kuwa kunapotokea moto katika maeneo yao wakishindwa kuwakamata wahalifu wao watawajibika kulipa faini ya uharibifu wa mazingira ya kuanzia shilingi 500,000/-.

Utamaduni wa uchomaji moto ovyo katika Mkoa wa Tabora unaoenekana kama kama jambo la kawaida wengine wakitaka malisho mapya ya mifugo na mengine wakati wa kuandaa mashamba na wakati wa kulina asali.
Jambo hilo limekuwa likimuumiza kichwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati mwingine kulizamika kuamuka usiku kuwavizia watu wanaowasha moto ovyo.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Tabora ameziagiza Halmashauri zote mkoani kuhakikisha vitalu vya miti waliyotayarisha kwa ajili awamu ya pili ya upandaji mkoani hapa inayomiti ya kutosha kwa kadri walivyokubaliana.
Alisema kuwa Manispaa ya Tabora inapaswa kuhakikisha imeotosha miche 500,000, Nzega Mji na Wilaya miche 500,000 na nyingine zilizobaki 250,000 kila moja.

Mwanri idadi hiyo ni nje ya ile ambapo kila mkazi wa Tabora atakiwa kupanda au kupandiwa na mzazi wake kama ni mtoto miti miwili kila mmoja.

No comments:

Post a Comment