Tuesday, August 29, 2017

Cheka akata rufaa BMT kupinga matokeo




Meneja wa bondia wa Cosmass Cheka, Juma Ndambile (kulia) akizungumzia matatizo yaliyompata bondia wake.
Cosmass Cheka akizungumzia hatua aliyochukuwa ya kukata rufaa BMT kupinga kufungiwa na matokeo ya pambano lake dhidi ya bondia Haidary Mchanjo.
 


Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Cosmas Cheka amekata rufaa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupinga matokeo na adhabu ya kufungiwa miezi sita na faini ya Sh200,000 iliyotangazwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).

Cheka alisema hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa TPBC ilikuwa na njama dhidi yake ili kumtengenezea nafasi bondia Haidary Mchanjo katika ngumi za kulipwa nchini.

Alifafanua kuwa adhabu dhidi yake haikufuata sheria kwani kwanza hakupewa nafasi ya kusikilizwa kwa mujibu wa sheria, huku akimpa nafasi mwamuzi wa pambano hilo, Modest Rashid ambaye alitaka kupigana naye kuitwa na kujieleza katika kikao cha TPBC.

“Hata kwenye mahakama, lazima mtuhumiwa apewe nafasi ya kusikilizwa au kujitetea, mimi nilikuwa ulingoni na mwamuzi na mpinzani wangu Mchanjo, mwamuzi amenitolea maneno machafu sana, haikutosha akaamua kunikata pointi, niliandika barua ya kulalamika TPBC, hawajaniita na kuibuka na adhabu kwangu,” alisema Cheka.

Alisema kuwa pamoja na maamuzi hayo kutonifikia kimaandishi, nimeamua kuchukua hatua za haraka kwani tayari vyombo vya habari mbalimbali na mitandaa ya kijamii yamekwisha tangaza maamuzi hayo yaliyofanywa bila kufuata sheria kwani hawakunipa nafasi ya kusikilizwa kwa mujibu wa sheria.

Meneja wa bondia huyo, Juma Ndambile, alisema kuwa walichokifanya TPBC ni kumvunja nguvu bondia wake ili ashindwe kuendelea na mchezo wake.

Ndambile alisema kuwa TPBC ilionyesha nia ya kuhujumu matokeo hayo mapema kwa kuweka vipingamizi mbalimbali pamoja na kutakiwa kumlipa mwamuzi wa pambano wakati wao hawakuwa waandaaji.

“Niliwaambia kuwa pambano limeandaliwa na kampuni inayoiitwa dragon, sasa kwa nini mimi nilipe, pia niliambiwa nitafute hela ya glovu, niligoma, nadhani hiyo ndiyo imekuwa chanzo,” alisema Ndambile. Alisema kuwa ili kumpata mshindi sahihi, bora pambano hilo lilirudiwe ili mshindi apatikane kwa mujibu wa taratibu na siyo kwa njia iliyotumika ambayo lengo lake ni kuharibu rekodi na kutengenza za bondia mwigine

No comments:

Post a Comment