Friday, June 9, 2017

Mshindi wa Milioni 20 Arusha akabidhiwa mzigo wake

WAENDESHAJI wa Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku, jana wamemkabidhi zawadi yake jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa Arusha, Oscar Haule, huku wakijigamba kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwakwamua washiriki wao kwa kuwapa fedha zao haraka ili waziingize katika majukumu yao ya kiuchumi.Mbali na kumpa zawadi hiyo ya fedha taslimu mshindi huyo, Biko pia wametangaza kutoa jumla ya Sh Milioni 500 kwa washindi wao waliocheza Biko mwezi Mei.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Biko Tanzania, Charles Mgeta, alisema wanaamini kuwa kiasi cha pesa walichompa mshindi wao atazitumia vizuri katika kujiletea maendeleo kama ilivyokuwa dhamira ya kucheza Biko na kufikia kutoa Sh Milioni 500 kwa washindi wa mwezi Mei.

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko Oscar Haule mwenye fulana nyekundu akipokea hundi yake ya ushindi kutoka kwa Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Biko Tanzania, Charles Mgeta kulia akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa Milioni 20 wa Biko droo ya Jumatano Oscar Haule wa jijini Arusha mwenye fulana nyekundu.

“Tunampongeza Haule kwa kushinda donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Biko katika droo iliyochezeshwa juzi Jumatano, sambamba na kuwapongeza wote wanaocheza mchezo huu kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ikiwa ni 2456,” Alisema Mgeta.


Naye Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema mchezo wa Biko ni rahisi kucheza pamoja na kushinda, hivyo kila Mtanzania anapaswa kuanza kucheza ili aweze kuibuka na ushindi wa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku zawadi nono ya droo kubwa ya Jumapili hii ikiwa ni Sh Milioni 20 kama ilivyokuwa Jumatano iliyopita.

“Huu ni wakati wakutajirika kwa kupitia Biko Tanzania ambapo hakuna bahati nasibu inayolipa haraka kama Biko, hivyo Watanzania wanapaswa kutumia vyema fursa za uwapo wa bahati nasibu hii iliyojizolea umaarufu nchini,” Alisema Kajala.

Naye Mshindi huyo wa Arusha, Oscar Haule, aliwashukuru Biko kwa kumkabidhi fedha zake haraka, huku akisema kuwa ni wazi ujio wa bahati nasibu ya Biko umekuja kwa ajili ya kumuondolea ugumu wa maisha yake.

“Nashukuru Mungu kwa kunipa bahati ya ushindi wa Biko, hivyo nawakumbusha Watanzania wote nao kucheza Biko ili washinde kama nilivyokuwa mimi kwa sababu ndani ya mchezo huu hakuna kujuana bali bahati kwa wale waliocheza,” Alisema.

Hadi sasa Biko wameshatoa zawadi kwa washindi wa Mwezi Mei jumla ya Sh Milioni 500, huku mshindi wa Jumapili hii kwenye droo kubwa akitarajiwa kuibuka na Sh Milioni 20 sanjari na zawadi za papo kwa hapo zinazotolewa kwa kupitia simu za mikononi zilizotumika kuchezea mchezo wa Biko.

No comments:

Post a Comment