Thursday, April 27, 2017

MGODI WA BULYANHULU WAONESHA VIFAA NA MBINU ZA KISASA ZA UOKOAJI MGODINI

Maonesho ya wiki ya usalama na afya kazini yameendelea katika viwanja vya Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia umeonesha vifaa vya kisasa na mbinu mbalimbali wanazotumia katika uokoaji maeneo ya mgodini.

Mgodi wa Bulyanhulu unashiriki kwenye maonesho ya wiki ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) yakiwa na kauli mbiu ya “Ongeza wigo wa ukusanyaji na utumiaji wa takwimu za usalama na afya”
Afisa Physiotherapia mgodi wa Bulyanhulu Tumaini Sylivanus akiwaelezea wananchi waliotembelea banda la mgodi wa Bulyanhulu kuhusu namna TENS Mashine inavyotumika kusaidia kupunguza maumivu kwa mtu aliyeumia msuli na jinsi wanavyotoa huduma ya kwanza kwa wafanyakazi wanaoumia wakiwa kazini
Mkufunzi na Mkuu wa Kikosi cha Uokoaji mgodi wa Bulyanhulu Melick Mganilwa akielezea kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya kisasa vya kupumulia wakati wa dharura mgodini
Wananchi wakiwa wamejaa katika banda la mgodi wa Bulyanhulu ambapo maafisa waliobobea katika masuala ya afya na usalama mgodini wanaonesha mbinu wanazotumia kuimarisha afya na usalama kwa wafanyakazi mgodini
Kushoto ni Afisa Uokoaji mgodi wa Bulyanhulu Nuerick Nyambina akionesha namna wanavyookoa watu kwa kutumia kamba endapo wakizama kwenye mashimo marefu na kuumia sehemu za mwili mfano mgongo na shingo
Afisa Uokoaji mgodi wa Bulyanhulu Nuerick Nyambina akitoa elimu kwa wananchi jinsi ya kufanya uokoaji kwa kutumia kamba pale mtu anapozama kwenye shimo refu
Mwananchi akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Uokoaji mgodi wa Bulyanhulu Nuerick Nyambina
Afisa Uokoaji mgodi wa Bulyanhulu Abubakar Muba akionesha jinsi ya kunyanyua gari iliyozama/iliyopinduka kwa kutumia mfuko maalum wa kisasa (Lifter Bag) wenye uwezo wa kunyanyua kitu chenye uzito wa tani 58 (angalia hapo chini ya gari)
Afisa Uokoaji mgodi wa Bulyanhulu Abubakar Muba akielezea jinsi Lifter Bag inavyosaidia katika uokoaji wa gari
Afisa Uokoaji mgodi wa Bulyanhulu Abdul Gibu akieleza kwa wananchi waliombelea banda la mgodi huo kuhusu suti maalum(kushoto chini) inayotumika kupambana na kemikali kuokoa watu kutoka kwenye kemikali zenye sumu
Afisa Uokoji mgodi wa Bulyanhulu Shaban Shamba akionesha jinsi ya kuingia kwenye shimo refu kwa kutumia kamba ndefu wakati wa uokoaji
Afisa Uokoji mgodi wa Bulyanhulu Shaban Shamba akionesha jinsi ya kuingia kwenye shimo refu kwa kutumia kamba ndefu.Kulia ni wakazi wa Moshi Mjini wakiangalia mbinu hiyo ya uokoaji
Afisa Uokoaji mgodi wa Bulyanhulu Abubakar Muba akielezea namna ya kupambana na moto kwa kutumia blanketi maalum
Kulia ni Afisa Tiba ya Kisaikolojia kutoka AAR Bulyanhulu Mwamvita Pangamawe akielezea juu ya elimu ya usalama kwa wafanyakazi kuhusu afya ya akili na mazingira kwa wananchi waliotembelea banda la mgodi wa Bulyanhulu.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment