Monday, January 16, 2017

WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA WAHAKIKIWA KIGOMA

 Mkaguzi Mkuu wa Ndani Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe akimhudumia mstaafu wakati wa zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, linalofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Kigoma, Mkoani Kigoma.
 Baadhi ya Wastaafu Mkoani kigoma wakisubiri kuhakiki taarifa zao katika zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu wanaolipwa na Hazina, linaloendelea katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
 Bibi Lucy Suzereje aliyekuwa mtumishi wa chuo cha maendeleo – Kihinga Mkoani Kigoma, akiwa ameshika kitambulisho chake cha kustaafu akisubiri kuhakiki taarifa zake za kustaafu kwenye ukumbi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Kigoma.
 Bw. Jumanne Mtumwa Kiragu (aliyevaa kofia) ambaye alikuwa mtumishi wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Idara ya Magereza akitoa taarifa zake za kusataafu kwa Mkaguzi wa ndani wakati wa zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu Mkoani Kigoma.
 Mkaguzi wa ndani wa Manispaa ya kigoma vijijini Bw. Filbert Muhamba (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mstaafu katika zoezi la uhakiki wa taarifa za wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, linalofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma –Ujiji Mkoani Kigoma.
 Mwandishi wa Habari wa TBC Mkoani Kigoma Bw. Dotto Elias (Kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa baadhi ya wastaafu Mkoani Kigoma mara baada ya kukamilisha uhakiki wa taarifa zao.
 Mkaguzi Mkuu wa Ndani Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe akiongea na wahandishi wa Habari akielezea utaratibu unaotumika katika kuhakiki taarifa za wastaafu katika zoezi la uhakiki unaendelea katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma –ujiji.
 Mstaafu Bw. Maganga Patric akiongea na wahandishi wa habari kuhusu zoezi la uhakiki linaoendelea Mkoani Kigoma katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma –Ujiji.

(PICHA ZOTE NA Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango-WFM)

No comments:

Post a Comment