Monday, January 16, 2017

MAAFISA TEHAMA WA MAHAKAMA YA TANZANIA WAPEWA DARASA

NA MAGRETH KINABO – MAHAKAMA

Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga amewataka Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) wa Mahakama ya Tanzania kutumia elimu na ujuzi ili kuweza kutatua changamoto zilizopo kwenye masuala ya TEHAMA.

Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji huyo wakati akifungua mafunzo hayo ya muda wa wiki moja yaliyoanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambayo yanafanywa kwa ushirikiano wa Mahakama ya Tanzania na Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).

“Mnatakiwa kutumia elimu mliyonayo , ujuzi mtakaoupata ikiwemo kuwa wabunifu katika vitu vipya ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika mifumo ya TEHAMA, alisema Mtendaji Mkuu, Bw. Kattanga.

Aliongeza kuwa maafisa hao wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya kwa pamoja kwenye shughuli za mifumo ya TEHAMA. Pia aliwataka kutumia ujuzi watakaoupata kuwafundisha wengine.

Bw. Kattanga aliwataka maafisa hao kuwa na uweledi katika ya masuala ya Serikali Mtandao, kujituma kufanya kazi na kuacha tabia ya kulalamika ,ikiwemo kuwa na mtandao wa kubadilishana mawazo katika masuala ya kitaaluma.

Akitoa mada kuhusu Shughuli za Wakala ya Serikali Mtandao, Bw. Bakari alisema dhima yake ni kusogeza huduma za Serikali kwa wananchi kupitia dirisha moja, ili kuwezesha utendaji wa shughuli hizo kwa gharama nafuu , ubora , wakati na kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Alisema mfumo huo pia unasaidia kuboresha huduma za Serikali katika jamii.Mafunzo hayo yamehusisha maafisa TEHAMA 25 kutoka katika kanda zote za Mahakama ya Tanzania.
Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akifungua mafunzo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Maafisa TEHAMA kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania . Mafunzo hayo ni ya muda wa wiki moja yenye lengo la kuongeza ujuzi yameanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam na yanafanywa na Mahakama ya Tanzania kwa ushirikiano wa Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).
Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akifundisha wakati akifungua mafunzo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) ya muda wa wiki moja yaliyoanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam. Mafunzo hayo yenye lengo la kuongeza ujuzi yanafanywa kwa ushirikiano wa Mahakama ya Tanzania na Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).
Baadhi ya Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) wakiwa katika mafunzo ya muda wa wiki moja kuhusu kuwajengea uwezo na ujuzi kwenye masuala ya TEHAMA yaliyoanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam. Mafunzo hayo yanafanywa kwa ushirikiano wa wa Mahakama ya Tanzania na Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).
Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Bakari akitoa mada juu ya Serikali Mtandao wakati wa mafunzo ya Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania.Mafunzo hayo ni ya muda wa wiki moja yameanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam na yanafanywa kwa ushirikiano wa Mahakama na Tanzania Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).(PICHA NA MARY GWERA).

No comments:

Post a Comment