Thursday, January 5, 2017

SIHABA NKINGA AKUTANA NA WAZEE WA KOO TANO WILAYANI TARIME

Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na wazee wa kimila kutoka koo tano mkoani Mara ambapo amewapongeza kwa kazi ya kuelimisha jamii inayowazunguka juu ya madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike na tohara mara mbili kwa watoto wakiume, Katikati ni Mtumishi Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) Bi. Kambibi Kamugisha, kushoto ni Katibu Tawala Tarime Bw. John Marwa na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai.

Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore akiongea na na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ambapo alishauri serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.
Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias Maganya akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ambapo alimuomba Katibu Mkuu kuangalia uwezekano wa kuwezeshwa kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kimila kutoka koo tano za Bukenye,Nyabasi,Bukira,Butimbaru na Buhunyaga leo Mjini Tarime
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na watoto wa kike walio katika mradi unaotekelezwa na Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) wa kuwawezesha kijasiriamali watoto waliokimbia vitendo vya ukeketaji.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiagana na watoto wa kike walio katika mpango wa kuwezeshwa kijasiriamali na Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF)
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) na watoto wakike walio katika mradi huo.

Na Hassan Silayo-MAELEZO

Wazee wa Kimila kutoka Koo Tano Mkoani Mara wamemuomba Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kuwawezesha kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.

Akiongea wakati walipokutana na Katibu Mkuu aliyepo Wilayani Tarime Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias Maganya alisema kuwa walishapata elimu kutoka kwenye Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) na changamoto ni jinsi ya kuzifikia koo nyingine Mkoani huko ili kuwezesha kuondoa kabisa mila hiyo.

“Tumechoka vitendo vya ukatili kwa watoto na vitendo visivyoturishisha sisi kama wazee, tutafanya kila jitihada kuweza kuondokana na vitendo hivi, tunahitaji ushiriki zaidi wa serikali na asasi nyingine zishirikiane na CDF ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo tuliloliweka” Alisema Mzee Elias

Akitolea ufafanuzi suala hilo Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga amesema kweli upo umuhimu wa kutekeleza suala hilo la kupeleka elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili kuweza kuwasaidia watoto wakike.

Naye Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore ameishauri serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.

Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Sihaba Nkinga alitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Dawati la Jinsia katika wilaya hiyo na kujionea namna wanavyofanya kazi na jinsi wanavyokabiliana na changamoto mablimbali.

Aidha Bi. Sihaba aliwatembelea watoto wa kike waliopo katika mpango wa uendelezwaji kijasiriamali unaotekelezwa na Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) katika kata ya Manga Wilayani Tarime Mkoani Mara.

No comments:

Post a Comment