Thursday, January 5, 2017

MAMILIONI YA KUZIMA MWENGE SIMIYU YA JENGA SHULE YA WATOTO WA WAFUGAJI MALINYI

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Malinyi.

Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ni moja ya Wilaya mpya hapa nchini zilizoundwa kutokana na ukubwa wa mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuzidi kuongeza huduma za kiserikali kwa wananchi walio pembezoni hili kupunguza gharama za wananchi kutembea umbali mrefu.

Malinyi ambayo imezaliwa kutoka katika Wilaya Mama ya Halamashauri ya Wilaya ya Ulanga ambayo ilionekana kubwa kuliko kawaida na kushindwa kukidhi kuwahudumia wakazi wa malinyi kutokana na umbali wa kijiografia.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,Marcelin Ndimbwa, akikagua ujenzi wa madarasa ambayo yamejengwa kwa ajli ya watoto wa wafugaji Rumbanga.

Marceline Ndimbwa ni Mkurugenzi wa kwanza katika halmashauri hiyo mpya kuteuliwa na Rais wa awamu ya tano Daktari John Pombe Magufuli ili kuhakikisha maendeleo ya wilaya hiyo yanafanana na sehemu nyingine.

Ndimbwa amekuwa ni mkurugenzi wa halamashauri hiyo huku akikabiliana na changamoto kubwa ya mgogoro wa ardhi baina ya wakulima na wafugaji na changamoto ya miundombinu ya elimu katika jamii kubwa ya wafugaji.

Ndimbwa anasema kuwa Rumbanga ni moja ya maeneo ambayo hayapo mbali na mji wa Malinyi lakini yamekuwa na jamii kubwa ya wafugaji wa kabila la kisukuma huku wakiwa na changamoto ya kutokuwa na shule ya msingi, Sekondari na huduma za afya.

Ndimbwa anasema kuwa mbali na changamoto zote hizo lakini ameamua kuanza na changamoto kubwa ya kutokuwepo na shule ya msingi katika eneo hilo la Rumbanga.

“kiukweli hali sio nzuri katika eneo la Rumbanga kwani shule iliyopo ni ya nyasi ambayo imejengwa na wanakijiji wenyewe na aina walimu wa kufundisha zaidi vijana wawili ambao wamemaliza kidato cha nne na kuamua kujitolea katika kuwafundisha wadogo zao ambao wapo kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne”amesema Ndimbwa.

 Ndimbwa anasema kuwa mara baada ya kuona mazingira hayo wakaona ni ulazima wa kuamua kujenga shule hiyo kuwa ya kisasa kutokana changamoto ya umbali kufata shule ambayo ipo kilometa 34 kutoka hapo Rumbanga na wanafunzi hao kutakiwa kutembea kwenda na kurudi katika shule ya msingi Mwembeni hali iliyochangia watoto wengi kuacha masomo na watoto wa kike kupata ujauzito katikati ya masomo na kulazimika kuacha shule.

Anataja kuwa katika hatua za awali zilizochukuliwa na halmashauri yake katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na  sera ya Rais Magufuli ya kupata elimu bure na sio bure tu bali iliyobora kwa wanafunzi, Serikali ya Wilaya imeamua kubuni arambee kutoka kwa jamii ya wafugaji na kutenga fedha kadhaa kwa ajili ya kujenga majengo ya kisasa ya shule ya msingi Rumbanga ambayo imeanza kutokana na jitahada za watu wa jamii hiyo ya wafugaji.

“hatua ya kwanza niliyochukua ni kuchukua fedha za zilizotengwa kwa ajili ya kwenda Simiyu kuzima mwenge kiasi cha shilingi milioni 4 zipelekwe Rumbanga kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo hivyo kuongeza hali ya mwamko kwa wakazi wa kijiji hicho chenye jamii ya wafugaji” anasema Ndimbwa.

Ndimbwa anasema wanafunzi hawa pindi shule zitakapofungua awatasoma tena katika mabanda ya nyumba za nyansi kama ilivyokuwa awali hivyo watakingi katika madarasa ya kisasa kama ilivyo kwa watoto wengine wa Tanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi, Nasoro Liguguda amesema kuwa uamuzi huo wa mkurugenzi wa mtendaji wa halmashauri umekuja wakati muafaka kwani jamii kubwa ya watoto wa wafugaji walikuwa wakiteseka kwa kupata elimu bora kutokana na wao kupendelea kuishi pembezoni na kuanzisha miji mipya.

Anasema wafugaji hao ambao kwa sasa wameamua kuishi malinyi hapo ni vyema nao wakapata stahiki zao za huduma za jamii kama ilivyo kwa jamii ya wakulima hili kupunguza migogoro.

Nae katibu wa kamati ya ujenzi wa shule hiyo, Joseph Paschal wanashukuru halmashauri kwa kuweza kuwapatia fedha za kujenga shule hiyo ambayo ni tumaini jipya kwa wakazi wa Rumbanga .

Anataja kuwa wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakikumbwa na chngamoto nyingi wakati wa masika pindi wanapohitaji kwenda shule kutokana na kushindwa kuvuka mto Rumbanga ambao mara zote uwa unajaa maji hivyo kukusa masomo kwa kipindi chote.

Kwa upande wake mkurugenzi Ndimbwa amesema kuwa serikali imekwisha ridhia kuiweka shule hiyo katika mpango ujao wa bajeti lakini kwa sasa shule hii itakuwa kama shule dada ya shule ya miembeni mpaka hapo itakapo pata usajili kamili.

Hivyo ametaja wazi kuwa shule hiyo ambayo itakuwa na miundombinu ya kisasa na ujenzi wa choo bora ambacho kitajengwa sambamba na Zahanati ya Lumbanga ambayo itajenga jirani na eneo hilo la shule.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,Marcelin Ndimbwa, akikagua madarasa ambayo yamejengwa kwa ajli ya watoto wa wafugaji Rumbanga.
Mkurugenzi wa malinyi,Marcelin Ndimbwa, akionyesha choo kilichokuwa kikitumiwa na wanafunzi hao.
sehemu ya ubao wa kufundishia wa shule hiyo ya manyasi.
mkurugenzi wa malinyiMarcelin Ndimbwa akitoka darasani katika shule ya msingi Rumbanga.
Wanafunzi wakiwa darasani.

No comments:

Post a Comment