Wednesday, January 11, 2017

MISS UNIVERSE TANZANIA 2016 AONDOKA LEO KWA MASHINDANO

Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2017 Jihan Dimachk ameondoka leo alfajiri na ndege ya Oman Air
kuelekea Manilla nchini Philipines kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Miss Universe. 
Jihan Dimachk aliyetwaa taji la Miss Universe Tanzania mapema mwezi Novemba mwaka jana anaenda kuiwakilisha Tanzania akiungana na wenzake kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni kuwania taji hilo. 
 Jihan Dimachk ameondoka akiwa amejiandaa vyema ikiwemo kisaikolojia, kimazoezi na kimavazi akishirikiana na wataalam mbalimbali kutoka hapa nchini. 
 Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications  ambaye pia ndio Mkurugenzi na Muandaaji mkuu wa Kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amewashukuru wadau mbalimbali kwa kujitoa na kushiriki katika kuhakikisha mrembo wetu anatayarishwa vyema. 
Jihan ameandaliwa vyema na wataalam kutoka Nyanja mbalimbali Mfano Kwa upande wa kuweka mwili fit kiakili na kiafya Colloseum Gym & SPA walimfundisha katika kipindi chote cha maandalizi yake.
Kwa upande wa ngozi Mama Patricia Metzger wa Beauty and Clinic salon alishiriki katika kutibu uso wake na kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, wakati  Zurii house of Beauty walimkabidhi vipodozi ambavyo vitakwenda kumsaidia kipindi chote cha mashindano. 
Dashing Diva Beauty lounge wao walihakikisha nywele zake zinakidhi na kupata mahitaji yote muhimu. 
 Katika mashindano mrembo ataenda kushiriki katika mashindano matatu ambapo kuna Vazi la Taifa (National Costume) Vazi hili limetolewa na mbunifu mahiri wa Kitanzania Diana Magesa. Vazi la jioni limetolewa na Beauty Point Botique Diana Magesa vazi la Taifa (National Costume).
Mavazi mengine ya kiafrika  yametolewa na wabunifu wakongwe na maarufu hapa nchini ambao ni Ally Rhemtulah, Martin Kadinda, Jamila Swai, Sia Cotoure, UkTz Fashion, H&A na Kiki Fashion Mapambo ya shingo na hereni amepambwa na Mannyata na Agretifila halikadhalika picha zake zote za kitaalam ambazo zitatumika ndani na nje ya nchi zimepigwa na Ally Zoeb 
Mkurugenzi mkuu wa mashindano haya ameendelea kutoa shukrani zake za dhati na kuelezea kuutambua mchango mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali Colloseum hotel na African Wild Life foundations ambao mbali na kudhamini safari ya mrembo lakini pia walitoa kambi kwa ajili ya mrembo kujinoa na kupata mafunzo yake kwa utulivu. 
 Halikadhalika Jihan jana alikabidhiwa bendera ya Taifa katika office ya Mkurugenzi Mkuu kitengo cha sanaa na Bi.Joyce Hagu ambapo alimtakia mrembo safari njema na mafanikio katika mashindano haya. Bi.Joyce Hagu akimwakilisha Mkurugenzi mkuu wa sanaaa alisema, 
“Tunatambua katika mshindano kunakuwepo na changamoto nyingi ila sisi kama Wizara tunakuombea Mungu na tunakutakia kila la kheri na mafaniko.Tumekuamini na ukaipeprushe vyema bendera ya Tanzania”. 
 Miss Universe Tanzania ameenda kushiriki mashindano haya ambapo fainali yake itakuwa tarehe 29 mwezi wa Januari mwaka huu.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa Taifa la Tanzania pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Amanda Ole Sulul, 2009 Illuminata James, 2010 Hellen Dausen 2011 Nelly Kamwelu , 2012 Winfrida Dominique, 2013 Betty Omara, 2014 Nale Boniface, 2015 Loraine Marriot na 2016 Jihan Dimachk ambaye ndo anayekwenda kutuwakilisha mwaka huu. Jihan Dimachk ameondoka leo alfajiri na ndege ya Oman Air.  

No comments:

Post a Comment