Wednesday, January 11, 2017

KAMATI YA BUNGE YA PIC YATEMBELEA EPZA


  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda wa Uwekezaji (EPZA) Bw.  Lamau Mpolo akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakati Kamati hiyo ilipotembelea eneo hilo mapema leo.
   Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Kiwanda cha Tanzania Tooku Garments kilichopo eneo la EPZA Bw.  Bakanga Paul akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kiwanda hicho.
 Mwanasheria  wa Kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Bw  Ibrahim Gamba (kushoto) kilichopo eneo la EPZA akimuelezea Mwenyekiti wa Kamati ya ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma (PIC) Mhe Albert Obama akimuelezea jinsi uzalishaji wa nguo unavyofanyika Kiwandani hapo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kiwanda hicho.
   Wajumbe wa  Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma (PIC) wakiangalia shughuli za uzalishaji nguo zinafofanyika Kiwandani hapo.
  Msajili wa Hazina (kulia) Dkt Oswald Mashidano pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Mhe Albert Obama (katikati) wakiangalia jinsi shughuli za ushonaji nguo zinavyofanyika Kiwandani hapo.(Picha na Ofisi ya Bunge).


No comments:

Post a Comment