Friday, March 4, 2016

MWIGULU AANZA ZIARA NCHI NZIMA KUFUFUA VITUO VYA UTAFITI NA UZALISHAJI MBEGU

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Mwigulu Nchemba akizungumza na Makamu Mkuu wa chuo za SUA (Sokoine University of Agriculture) alipofika kwaajili ya kukutana na wataalam na uongozi wa SUA kwaajili ya kupokea maoni yao kuelekea kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa. "Transformation of Agriculture".
Katika kikao hicho,Wataalam kutoka SUA walisisitiza kuwa ili Tanzania iweze kuondokana na kilimo holela,ni wakati muafaka sasa kama nchi kuamua kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji na kuondoakana na kilimo cha mvua,pia kuachana na jembe la mkono na wakati huo huo kuimarisha vituo vya utafiti na kuzalisha mbegu kikanda.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia mfereji ulioandaliwa kwaajili ya kusambaza maji kwenye shamba la utafiti wa mbegu za Mpunga-Kilombero.Matumizi ya mifereji kwenye kilimo yanaondoa mfumo wa kutegemea mvua ili mimea kupata maji na kukua kwa wakati. Mwigulu Nchemba anatarajia kuendelea na ziara ya kukagua vituo vya Utafiti na uzalishaji wa mbegu nchi nzima,lakini wakati huo huo atatembelea mashamba ya mifugo na maeneo ya uvuvi wa samaki.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo na mtafiti wa mbegu kutoka mmoja ya maafisa wa juu wa wakala mkuu wa aghala la mbegu za ASA(Agricultural Seed Agency) Mkoani Morogoro.Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akikagua mbegu zilizopo kwenye ghala la ASA mkoani morogoro.Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na watumishi wa ASA(Agricultural Seeds Agency) wakati wa ziara hiyo,Kubwa alilosisitiza ni uzalendo na kufanya kazi kwa kujituma.Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kuhusu malisho ya ng'ombe yanayopatikana kwenye kituo cha utafiti wa mifugo -Morogoro(LITA).Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia baadhi ya ndama wa Ng"ombe waliopo kwenye shamba la Utafiti kwenye kituo cha LITA-Morogoro.Picha/maelezo na festo Sanga Jr

No comments:

Post a Comment