Tuesday, October 6, 2015

SIKU YA 2 :BENKI YA CRDB TAWI LA WATER FRONT WAENDELEA KUADHIMISHA WIKI HUDUMA KWA WATEJA

Meneja wa Benki ya CRDB wa tawi la Water Front, Donath Shirima akimpa tunzo pamoja na barua ya kumshukuru Afisa Mtendaji  mkuu wa Mohamed Interpraises, Mo dewji  kuwa ni mshiriki mkubwa wa benki ya CRDB katika tawi la Water Front leo katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika ofisi za Melt  jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji  mkuu wa Mohamed Interpraises, Mo dewji  akionyesha barua ya kumshukuru aliyopewa na Meneja wa Benki ya CRDB wa tawi la Water Front, Donath Shirima leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya CRDB wa tawi la Water Front, Donath Shirima akimpongeza Mo Dewji (kulia) kuwa ni mshiriki mhimu sana katika benki hiyo tawi la Water Front ndio maana wameona vyema kumpongeza kwa ushiriki wake ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam katika tawi hilo.
Kushoto ni Meneja wa mikopo benki ya CRDB tawi la Water Front, Isaya Lyimo na Meneja wa biashara wa benki ya CRDB tawi la Water Front, Adam  Akaro wakimsikiliza Afisa Mtendaji  mkuu wa Mohamed Interpraises, Mo dewji  alipotembelewa leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 
Meneja wa Benki ya CRDB wa tawi la Water Front, Donath Shirima akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea ofisi ya Afisa Mtendaji  mkuu wa Mohamed Interpraises, Mo dewji leo jijini Dar Es Salaam.
HUDUMA YA AFYA KWA WATEJA NA WAFANYAKAZI.
Meneja wa biashara wa benki ya CRDB tawi la Water Front, Adam  Akaro akipima shinikizo la damu, (BP) leo katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja inayoendelea kufanyika jijini Dar Es Salaam, ikiwa wateja wa tawi hilo wanakipimwa shinikizo la damu, urefu na uzito na hospitali ya AAR City center.
Mteja wa benki ya CRDB tawi la Water front akipima urefu leo jijini Dar es Salaam.
Mteja wa benki ya CRDB tawi la Water front akipima akipima Shinikizo la Damu leo jijini dar es Salaam katika tai hilo.
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Water Front wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment