Tuesday, October 6, 2015

MKUTANO WA PILI WA MWAKA WA KIMATAIFA WA WATAALAM WA KUDHIBITI MBU WAFUNGULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

MKURUGENZI  Mkuu wa Taasisi ya Utafiti  wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), Dk. Mwele Malecela akifungua mkutano huo wa pili wa mwaka wa kimataifa wa wataalam wa kudhibiti Mbumbu kwa Nchi zisizofungamana Afrika (PAMCA) ulioanza leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mkutano huo umeshirikisha Wanasayansi watafiti kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa PAMCA ulifanyika jijini Nairobi Kenya 2014.

Dk Malecela amesema kuwa mkutano huu unakutanisha wataalam wa kupambana na Mbu Afrika nzima wataweza kukaa na kubadilishana uzoefu wao juu ya njia za kupambana na mbu.

“Wataalam hawa wanakutana kupitia umoja wao wa PAMCA utawawezesha wataalam hawa kujadiliana njia mbalimbali za kuweza kupambana na mbu hasa kutokana na tabia za mbu za kubadilika badilika na kufanya kuwa sugu kwa madawa mbalimbali,”alisema Dk Malecela.

Amesema wataalm wa Mbu wanapokutana katika mikutano kama hii huwawezesha wataalam kupata ujuzi mpya wa kuweza kupambana na kukabiliana na mbu.

Mbu huambukiza magonjwa mengi, hivyo kuwa na taasisi ya wataalm wa Waafrika wenyewe ni jambo la kujivunia sana hivyo mkutano huu utaweza kufanikisha kupata vitu mbalimbali kutokana na mada zitakazo wasilishwa na ambazo zitaingizwa katika mipango na sera mbalimbali katika nchi zetu.
Mapema akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa  Kimadawa Kenya (KEMRI), Musau Kyanesa amesema lengo la kuanzishwa kwa PAMCA ni kutafuta njia stahiki ya kupambambana na mdudu mbu ambae hueneza magonjwa mbalimbali ambayo huathiri binadamu.



“Itakuwa ni jambo jema sana kama tutaweza kumdhibiti mdudu huyu mbu ambaye anaeneza magonjwa haya na kufanikiwa kwa hilo tutaweza kuendeleza afya za wananchi wetu kwa nchi za Afrika, maana Afrika ndio tunapata shida sana na mdudu huyu mbu,” alisema Kyanesa.

Aidha Kyanesa ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa KEMRI amesema wameandaa mpango wa kuhamasisha wanafunzi vyuoni kujikita katika sayansi ya Mbu ili kupata watalaam wengi wakuweza kukabiliana mbu Kenya na Afrika kwa ujumla. 

"Tunaandaa mpango wa kuhamasisha vijana kusomea na hatimaye kuwa na utaalm juu ya mapambano na kufanya tafiti za mbu, kwa kugharamia masomo yao kutokana na upungufu wa wataalam kulingana na tatizo lenyewe,"alisema Kyanesa.

 Mwenyekiti wa Bodi ya PAMCA, Prof Charles Mbogo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo.
 Washiriki wakisikiliza mada mbalimbali katika siku ya kwanza ya mkutano huo, Dar es Salaam leo.
 Rais wa PAMCA tawi la Tanzania, Dk Stephen Magesa akizungumza katika mkutano huo.
 Mkuu wa NIMRI Tanzania, Dk. Mwele Malecela akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa KEMRI kutoka Kenya, Musau Kyanesa baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
 Prof Wen Kilama akiwasilisha mada juu ya Maadili ya Utafiti wa Afya hususani Maleria Afrika .
 Prof Wen Kilama akiendelea na uwasilishaji wa mada yake. Prof Kilama ni Mkurugenzi Mstaafu wa NIMR.
 Dk Mwele Malecela na washiriki wengine wakifuatilia mada ya Prf Kilama.
 Washiriki wakifuatilia mada hiyo.
Picha ya pamoja ya washiriki mkutano huo wakiwa na mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment