Monday, September 21, 2015

NAIBU WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR ISSA USI GAVU AFUNGUA MKUTANO WA MAADHIMISHO YA SIKU YA BAHARI DUNIANI UNAOFANYIKA KITAIFA MKOANI MTWARA LEO MCHANA

Sehemu  ya wajumbe wa Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika Kitaifa mkoani Mtwara,leo mchana, wakisikiliza mada mbalimbali zinazohusu changamoto na mikakati ya kuboresha mazingira ya Usafiri wa Majini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, akitoa shukrani zake kwa Ushirikiano unaoonyeshwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika sekta ya Uchukuzi kabla hajamkaribisha Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano kufungua rasmi  Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika mkoani Mtwara,leo mchana.
 Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande, akifafanua jambo katika Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika mkoani Mtwara, leo mchana.
 Mkuu wa Kikosi cha Meli Vita (701 KJ), TPDF-NAVY, Brigedia Generali, Richard Makanzo, akifafanua jambo, leo mchana katika Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika Kitaifa mkoani Mtwara, leo mchana
Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Zanzibar, Issa Usi Gavu, akifungua rasmi Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika mkoani Mtwara,leo mchana.Maadhimisho ya Siku ya Bahari yanafanyika Kitaifa Mkoani Mtwara kwa siku tatu. 
(Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

No comments:

Post a Comment