|
Balozi Dr Mahiga -Iringa mjini.
Na matukiodaimaBlog
ALIYEKUWA balozi wa kudumu wa umoja wa mataifa (UN) na mgombea urais katika mchakato wa ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) balozi Dr Augustono Mahiga anayeomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM amewashangaa makada maarufu wa chama hicho walioshindwa katika mchakato wa ndani ya chama kwa nafasi ya urais kuhama chama hicho kuwa hao hawakuwa na mapenzi ya kuwatumikia watanzania na kuwa watazunguka kote ila chama makini ni CCM pekee na kuwataka wana CCM jimbo la Iringa mjini kumpa nafasi yeye ili kuondoa masalia ya Chadema .
Balozi Dr Mahiga alisema kuwa wana CCM hao walioanza kuhama chama kwa kukosa nafasi ya urais hawakuwa na mapenzi mema na CCM bali walikuwa wawametanguliza maslahi yao mbele na kuacha kuangalia maslahi ya Taifa na chama hivyo ni vema watanzania kuwatazama kwa jicho la tatu na ikiwezekana kuwachunguza japo kwa miaka 5 bila kuwachagua kuwa viongozi wao.
Alisema kuwa kama suala ni uongozi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na chama kulikuwa hakuna sababu ya kuhama chama ama kuanza kutukana chama kwa sasa ila wangeweza kushuka chini na kugombea nafasi za chini ukiwemo udiwani ama ubunge kama ambavyo yeye alivyoshuka na kugombea ubunge ili kuwatumikia watanzania kwa ngazi ya ubunge.
"Kila nafasi ndani ya chama ina maana kubwa katika kutumikia watu hivyo kuhama chama si jambo jema na upande wa vyama lazima kuwa makini na wanachama wanaohama vyama kwa sasa ili kupata nafasi za uongozi iwapo watakosa nafasi hizo bila shaka watachukua hatua ya kuvuruga nguvu ya vyama hivyo ama kuhama vyama "
Balozi Dr Mahiga aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa kuhusiana na mchakato mzima wa kumpata mgombea Urais wa CCM Dr John Magufuli na mchakato wa kura za maoni katika ngazi ya udiwani na ubunge katika jimbo la Iringa mjini ambako ni mmoja kati ya wana CCM 14 wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea wa ubunge .
Alisema akiwa kati ya wana CCM 41 waliojitokeza kuchukua fomu ya Urais hana kinyongo na uteuzi wa mgombea Urais wa CCM Dr Magufuli kwani ni mtu makini na safi ambae viatu vya Rais wa awamu ya nne Dr Jakaya Kikwete ataweza kuvimudu vema kutokana na kutokuwa mtu wa kulipisha kisasi na hana makuu na mtu zaidi ya kulitumikia Taifa .
Hivyo alisema iwapo wana CCM jimbo la Iringa mji watamchagua yeye kuwa mgombea ubunge jimbo hilo wawe imani ya kulikomboa jimbo hilo asubuhi saa 12 kutoka kwa Chadema chini ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa kwani alisema si kweli kama Chadema Iringa mjini wananguvu kubwa kuliko ya CCM na ukitazama idadi ya wenyeviti wa mitaa ambao CCM inao wenyeviti 104 huwezi linganisha na wale 64 wa Chadema kabla ya wenyeviti wake 13 kuvuliwa nafasi zao na mahakama.
Alisema dawa ya ushindi wa kishindo kwa CCM Iringa mjini ni moja pekee kuvunja makundi na kuwa kundi moja la ushindi baada ya zoezi la kura za maoni kumalizika .
|
|
Dc Mwamoto kulia akiwa na mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa ,mwamoto ni mgombea ubunge Kililo
Mkuu wa wilaya ya Kaliuwa mkoani Tabora Bw Venance Mwamoto ambae anawania kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Kilolo mkoani Iringa amesema kuwa tishio la kutaka kuuwawa kwake majuzi baada ya kufyatuliwa risasi katika gari lake wakati akitoka katika kampeni kata ya Ilula bado haimtishi katika safari yake ya kuwatumikia wananchi wa jimbo la Kilolo linaloongozwa na Prof. Peter Msolla .
Kwani alisema moja kati ya ahadi yake kubwa kwa wananchi wa Kilolo ni kuona amawatumikia kwa kasi zaidi na kumaliza kero ya maji katika mji wa Ilula na changamoto nyingine ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi kilichopita na mbunge aliyekuwepo .
Mwamoto alisema kuwa kazi nzuri aliyoifanya kwa nafasi ya ukuu wa wilaya kwa kipindi kifupi ambacho Rais Dr Jakaya kikwete alipomteua kwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kibonde na Kaliuwa ni wazi ni kipimo tosha na heshima kubwa ya wananchi wa Kilolo kujivunia na wategemee makubwa zaidi iwapo watamchagua kuwa mbunge wao kwa sasa .
|
waziri Lukuvi - Isimani
Mbunge wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi amewaomba wananchi wa jimbo hilo hasa wanachama wa CCM kuendelea kujenga imani kwake na kuwa ndani ya CCM kuna Demokrasi na kila mwanachama ana sifa ya kugombea nafasi yoyote ndani ya chama japo kipimo cha kuchaguliwa bado kipo kwa wananchi wenyewe ambao wanaweza kumpima kwa kazi alizofanya badala ya kushawishiwa kwa manenio bila vitendo.
Lukuvi ambae ni waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema kama si wana Isimani kuonyesha ushirikiano wao kwake na hata kumchagua katika nafasi hiyo ya ubunge basi heshima ambayo ambayo wana Iringa wameipata kupitia wizara yake leo isingekuwepo .
Alisema suala la migogoro ya ardhi amepata kulishughulikia kwa umaniki mkubwa na kuwa sulaa hilo pia lilikuwa ni kero kubwa hata kwa wananchi wake wa jimbo la Isimani ila kwa sasa kwa kiasi limeanza kupungua na kuwa iwapo wataonyesha imani yao tena wategemee kuona maendeleo makubwa zaidi katika jimbo hilo na kutaka baadhi ya kazi kubwa ambazo zimefanyika kuwa ni pamoja na barabara ya lami ya Iringa- Dodoma, umeme vijini , ujenzi wa shule pamoja na ujenzi wa nyumba bora kwa kupata bati za ruzuku .
"Tumekuwa pamoja muda wote katika maendeleo na matatizo hivyo lazima kila safari ina wasindikizaji wake na siku zote penye maendeleo ndipo panapopendwa na wengi ila bado kwa tathimini yetu Ismani ya leo sio ya jana . nimekomesha ulanguzi wa mazao kama mpunga ,alizeti kwa kufunga mashine"
Godfrey Mgimwa -Kalenga
Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa anayeomba kuteuliwa tena kuwa mgombea wa CCM nafasi ya ubunge amewashukuru wananchi wa kalenga kwa kuonyesha ushirikiano kwake na kuwa hadi sasa amepata kutekeleza ahadi zake kwa wananchi kwa asilimia 99 na kuwa zipo changamoto mbali mbali ambazo watampa tena nafasi ya ubunge atakwenda kuzifanyia kazi .
Mgimwa ambae amepata kuongoza jimbo hilo kwa mwaka mmoja pekee akichukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dr Wiliam Mgimwa aliyefariki duni mwaka jana mwanzioni ,alisema zilikuwepo ahadi mbali mbali ambazo ziliachwa na mbunge aliyepita na tayari zote amezikamilisha kwa kipindi cha mwaka mmoja na kubwa anajivunia kuanzisha vikundi vya Vicoba zaidi ya 60 ,ujenzi wa barabara , maji vijiji ,umeme na uchangiaji wa ujenzi wa zahanati ,shule na maabara na kuwa zaidi ya Tsh milioni 100 amepata kutumia kwa kuchangia miradi ya maendeleo jimboni.
Wewe Mahiga unaweza ukatumikia nchi kwenye chama chochote kile siyo lazima kiwe CCM, Nchi na chama ni vitu viwili tofauti. Waliohama chama wanatekeleza demokrasia na ni haki yao ya msingi kama vile wewe ukivyotafuta opportunity ya kuwa mbunge baada ya kushindwa kwenye urais. Hao wanaohama wanayo akili timamu, wewe kama umeamua kubaki CCM ni uamuzi wako ndiyo maana hakuna anayekuingilia au anayekusema vibaya, hivyo na wewe uache kuwasema vibaya wenzako wanaohama ndiyo maana kuna vyama vingi. Kumbe ungekuwa rais ungekuwa na closed mind.......si lazima kila mtu afanye wewe unavyoona ni sawa au afikiri wewe unavyofikiri. Nategemea utanielewa daktari.
ReplyDelete