Na Asteria Muhozya, Tanga
Kufuatia kuongezeka kwa kiwango cha mafuta yanayoingizwa nchini kupitia mfumo wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja nchini (BPS), bandari ya Tanga itakua bandari ya pili kupokea shehena ya mafuta kwa kutumia mfumo huo.
Hayo yameleezwa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati wa kikao baina yake Uongozi wa Mkoa wa Tanga, Taasisi za Serikali zinazoshughulika na masuala ya mafuta na wadau wa mafuta mkoani Tanga.
Aidha, Waziri alirejea kauli yake wakati akikagua miundombinu ya kuhifadhi mafuta katika Bohari ya kampuni ya GBP na kampuni ya TSN group wamiliki wa bohari ya TAPCO.
Akizitaja faida za kutumia bandari hiyo ameeleza kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa uhakika wa upatikanaji na usambazaji mafuta, kupunguza msongamano uliopo kwa kutegemea Bandari ya Dar es Salaam, kupunguza gharama za usambazaji mafuta ikiwemo kukuza uchumi wa Mkoa wa Tanga na hivyo kuchangia zaidi katika Pato la taifa.
Akiongea katika kikao hicho, Simbachawene amesema hiyo ni fursa nzuri kwa serikali na itashirikiana vizuri na kwa kwa karibu na wadau wote walio tayari kufanya kazi katika eneo hilo, na kuutaka mkoa huo kuipokea shughuli hiyo kikamilifu kwani ni sehemu ya mafanikio ya mkoa huo.
“Kila mdau anahusika katika suala hili, faida kwa Mkoa huu ni kubwa zaidi, zipo faida za kiuchumi na kijamii, lakini pia usalama wa mafuta nchini, mazingira ya sekta hii yamekua mazuri, ndio maana wenzetu jirani wanapitia bandari ya Dar es Salaam, Tanga itasaidia zaidi katika kufanikisha mafanikio haya”,ameongeza Simbachawene.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni GBP ya Tanga, Badar Masoud (katikati),
akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene, (kulia) kutembelea
Bandari ya Tanga itakayotumika kwa katika shughuli za kushusha mafuta jijini humo.
Wengine nyuma ni wadau wa Mafuta Tanga,
na Uongozi wa Mkoa wa Tanga.
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene (wa pili kushoto) akikagua
miundombinu ya kuhifadhi mafuta katika Bohari ya Kampuni ya GBP ya Tanga. Nyuma ya Waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula. Wengine kutoka
kulia ni Meneja Mkuu wa PICL, Michael Mjinja, Kamishna wa Nishati na Maendeleo
ya Petroli Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi, Hosea Mbise na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya GBP ya Tanga, Badar Masoud. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
GBP, Bohari hiyo ina uwezo wa kuhifadhi lita milioni 26 za mafuta.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya GBP ya Tanga, Badar Masoud
akimwonesha akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene
wakati akikagua miundombinu ya kuhifadhi mafuta katika Bohari ya Kampuni
ya GBP , Tanga. Wengine katika picha ni
Baadhi ya watendaji wa Wizara na wadau
wa mafuta mKoa wa Tanga zikiwemo Taasisi za Serikali.
Mhandisi katika Kampuni ya TSN Group, ambao ni wamiliki wa bohari ya kuhifadhi mafuta ya TAPCO Mhandisi
Michael Shimiu,(wa tatu kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene (wa pili kushoto) na ujumbe wake wakati walipoitembelea
Kampuni hiyo kuona miundombinu ya kuhifadhi mafuta ya Kampuni hiyo. Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Said Magalula na kulia ni Mkurugenzi wa TSN Group, Farouk
Baghoza.
Meneja Biashara sehemu ya Mafuta ya Petroli wa Kampuni ya Lake Gas,
Jamal Yahaya, akimwonesha Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene na ujumbe wake, Matanki ya kuhifadhi gesi ya kampuni hiyo (hayapo
pichani) wakati Waziri alipotembelea kampuni
hiyo mkoani Tanga.
Baadhi ya Matanki ya kuhifadhi mafuta ya kampuni ya TSN Group,
wamiliki wa Bohari ya TAPCO.
Sehemu ya wadau wa mafuta mkoa wa Tanga, wakifuatilia kikao baina ya
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene, Uongozi wa Mkoa wa Tanga na
Taasisi za Serikali zinazosimamia masuala ya mafuta nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula, akiongea jambo wakati wa kikao
cha majumuishi baina ya Mkoa wa tanga Wizara ya Nishati na Madini, Taasisi za
Serikali zinazohusika na masuala ya mafuta na wadau wa mafuta Mkoa wa Tanga.
Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said
Magalula na wa kwanza Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza.
Meneja Mkuu wa PICL, Michael Mjinja (wa pili kulia), akiongea jambo
wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kushoto)
alipotembelea Bohari ya Kampuni ya GBP ya Tanga, kukagua miundombinu ya
kuhifadhi mafuta ya kampuni hiyo. Wa Pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Said Magalula,wa tatu kulia ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli,
Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi, Hosea Mbise, katikakati ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni GBP ya Tanga, Badar
Masoud
No comments:
Post a Comment