Baadhi ya wateja wa Benki ya
CBA Tanzania wakipakua chakula cha futari iliyoandaliwa kwa ajili yao kwenye
hoteli ya serena mwishoni mwa wiki
Wateja wa Benki ya CBA
Tanzania wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili yao kwenye
Hoteli ya Serena Mwishoni mwa wiki .
Mkurugenzi wa Benki ya CBA
Tanzania Julius Mcharo akiongea na wateja na wafanyakazi wa benki hiyo
waliohudhuria futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwenye hoteli ya Serena
mwisoni mwa wiki
.MkurugenzI na Maofisa waandamizi wa benki hiyo katika picha ya pamoja baada ya
futari hiyo
*********
Benki ya CBA Tanzania leo
imewafuturisha baadhi ya wateja wake wa jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya
kuboresha uhusiano na wateja ambapo pia itawaandalia wateja wake futari
kwenye maeneo mbalimbali iliko na matawi nchini .
Akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na CBA Tanzania kwa wateja katika
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Bw.Julius
Mcharo alisema “ Tunawashukuru sana wateja wetu nchini kote kwa kuendelea kuiamini
benki yetu katika kupata bidhaa na huduma za kibenki na ndio maana
tunashirikiana nao sana katika maeneo maalum ambayo yanatukutanisha ili pia
tuweze kujadiliana na kuboresha ushirika wetu kama tunavyokutana leo kwenye
futari hii”.
Alisema Benki ya CBA Tanzania huwa inakutana na kushirikiana na wateja wake
katika masuala mbali mbali ya jamii ikiwemo michezo burudani na hata katika
matukio ya kuchangia kuinua sekta mbali mbali mfano afya na elimu. “Lakini leo
ni siku muhimu kwetu hapa Dar es Salaam kwa kuwa tunafuturu pamoja na kutakiana
mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani ambao unaendelea”.
Bw.Mcharo aliahidi kuwa Benki itaendelea kuboresha bidhaa na huduma zake ili
ziendelee kuwa na ubora wa hali ya juu kabisa ikiwa ni pamoja na kubuni huduma
mbalimbali za kuwarahishia maisha wateja wanapohitaji kupata huduma za kibenki
na kuboresha shughuli zao.
“Benki ya CBA Tanzania tunawatakia mfungo mwema wa Ramadhani lakini pia
maandalizi mema ya sikukuu!, endeleeeni kufurahia huduma zetu mbalimbali na
msiache kutembelea matawi yetu au kutembelea mtandao wetu kwa njia ya
kisasa ya kuona huduma zetu mbalimbali kama vile huduma ya mkopo wa bima
ambayo inaonekana kuwa mkombozi kwa watu wengi,mikopo ya kununua nyumba yenye
masharti nafuu pia tunatoa huduma ya M-Pawa kwa kushirikiana na Vodacom
inayowezesha wateja wa M-Pesa kuweka akiba na kupata mikopo kwa haraka na bila
masharti magumu.” Alisema
Benki ya CBA Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia uboreshaji wa
maisha ya jamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za
miradi ya maendeleo.Bado CBA ina mpango wa kutoa misaada katika mikoa ya
mbalimbali kwa dhumuni la kuendelea kupunguza tatizo la kipato kwa wananchi
wanaoishi katika mazingira magumu.
CBA Tanzania ni sehemu ya CBA Group iliyopo
katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania,
CBA Tanzania ina matawi kumi na moja, iko katika mikoa ya mwanza, Moshi,
Arusha, Mtwara, Mbeya na Tunduma.
No comments:
Post a Comment