Friday, June 5, 2015

PSPF YATOA ELIMU YA MFUKO KWA WAHESHMIWA MABALOZI, WAHAMASIKA WAJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Memba (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Adam Mayingu, baada ya kikao cha waheshimiwa Mabalozi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa tatu kulia) akimpongeza Costantin Martin, Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF baada ya kutoa mada kwa waheshimiwa mabalozi.

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Balozi John Haule akipata maelezo juu ya PSPF kutoka kwa Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF Costantina Martin.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Peter Kallaghe akijaza fomu ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, anayeshuhudia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Abdul Njaidi.


Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Radhia Msuya akijaza fomu ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, wanaoshuhudia ni Maafisa wa PSPF, Hadji Jamadaly (katikati) na Zuhura Lwamo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) kipata maelezo juu ya michango katika PSPF kutoka kwa Afisa wa PSPF Easter Jorry.

Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi, Costantin Martin akitoa mada ya Mfuko kwa waheshimiwa mabalozi wa Tanzania wanaiwakilisha katika nchi mbalimbali.


Hivi karibuni Mfuko wa Pensheni wa PSPF ulitoa semina kwa waheshimiwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

Katika semina hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Ramada, jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF Costantina Martin alipata fursa ya kutoa mada juu ya PSPF.

Mada ya meneja huyo wa PSPF ilijikita katika maeneo yafuatayo; historia ya PSPF, wanachama wa PSPF, Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, mpango wa lazima, mafao yatolewayo na PSPF, mikopo itolewayo na PSPF, kikokotoo cha mafao, uwekezaji, huduma kwa wateja, utunzaji wa kumbukumbu kwa wanachama, mafao yaliyolipwa kwa wastaafu, wastaafu na thamani ya Mfuko.

Baada ya mada hiyo waheshimiwa mabalozi walihamasika na uimara wa Mfuko na hatimaye wengi kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari

Kiwango cha uchangiaji katika mpango wa uchangiaji wa hiari ni kuanzia shilinghi 10,000/- au zaidi. Michango itawasilishwa moja kwa moja kupitia akaunti ya benki au wakala wa malipo wa M-Pesa, Tigo-Pesa, Airtel-Money au Maxmalipo.

PSPF ilianzisha mpango huu ili kuhakikisha kila mtanzania anafaidika na Hifadhi ya Jamii, PSPF kupitia mpango wake wa Uchangiaji wa Hiari tumeendelea kusajili watanzania na wasio watanzania ambao wanaishi nchini katika mpango huu, pia tunatoa huduma hii hata kwa watanzania wanaoishi nje ya Tanzania, lengo hapa ni kuhakikisha kila mtanzania anakuwa salama katika Hifadhi ya PSPF. Lengo la mpango huu ni kupanua wigo wa wanachama kwa kuandikisha wananchi waliojiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi.

No comments:

Post a Comment