Saturday, April 11, 2015

Balozi Seif Idd afungua Mafunzo ya Miezi Mitatu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali wakati wa hafla ya kuyafunga mafunzo hayo hapo Skuli ya Sekondari Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kati kati yao ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mheshimiwa Sadifa Juma Khamis, na nyuma ya Balozi Seif ni Mratibu wa Mradi unaoondesha mafunzo hayo Nd.Abdi Hamid Abeid.
Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali akimpatia maelezo Balozi Seif wakati alipotembelea Darasa la mafunzo hayo hapo Skuli ya Sekondari Donge.
Baadhi ya Wanafuzi wa Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar wakishuhudiwa na Balozi Seif wakiendelea kufanya mazoezi ya vitendo katika kukabiliana na matatizo madogo madogo yanayojichomoza wakati wa matumizi wa kompyuta zao.
Mmoja wa Wanafunzi wa Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar akiperuzi kuangalia nini kimejiri duniani kupitia mtandao wa Internet akishuhudiwa na Balozi Seif.
Baadhi ya Wananchi na Wanafunzi wakisikiliza Hotuba ya Mgeni rasmi Balozi Seif hayupo pichani wakati akiyafunga mafunzo ya miezi mitatu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar hapo Skuli ya Sekondari Donge.
Balozi Seif akimkabidhi Cheti Mwenyekiti wa Jumuiya Kupambana na changamoto na kuwaendeleza Vijana Zanzibar Bibi Umukulthum kwa kusaidia uendeshaji wa mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano. Kati kati yao ni Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar Maalim Khamis Mussa, na kushoto ya Balozi Seif ni Mratibu wa Mradi wa Mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano Abdi Hamid Abeid na Mkuu wa Mafunzo hayo Nd. Abdulla Othman Ali.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jimbo la Donge, walimu na wanafunzi wa mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano yaliyokuwa yakifanyika katika skuli ya Sekondari ya Donge. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwakilishi wa Jimbo la Donge ambae pia ni Waziri wa Elimu Mh. Ali Juma Shamuhuna, Mratibu wa Mradi wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Abdi Hamid Abeid na Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZAFAYCO Bibi Umukulthum. Kulia ya Balozi Seif ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis, Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar Maalim Khamis Mussa. Picha na – OMPR – ZNZ.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaasa Vijana wanaojifunza Taaluma ya Mitandao ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuwa makini katika matumizi bora ya mfumo huo mpya ili kulinda mila na Tamaduni zao za asili.

Alisema si vyema kuthubutu kufanya matumizi maovu way mfumo huo akijua kwamba yatawashawishi kujiingiza katika matendo yatakayowapelekea kuwa na maamuzi ya kufanya vitendo vilivyo nje ya utamaduni wao.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akiyafunga Mafunzo ya Miezi Mitatu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar { TEKNOHAMA } yaliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar { UMUZA } na Jumuiya ya kupambana na changamoto na kuwaendeleza Vijana Zanzibar { ZAFAYCO } hapo katika Majengo ya Skuli ya Sekondari Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema Dunia imekuwa na Mabadiliko makubwa ya Teknolojia ya Kisasa ya Mawasiliano inayokwenda kwa haraka kiasi kwamba Jamii za Kimataifa popote pale zilipo hupata fursa za kuwasiliana, kushirikiana na hata kupashana taarifa kupitia mfumo huo.

Akisoma Risala Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nd. Abdullah Othman Ali alisema kwa kuelewa matatizo na changamoto zinazowakabili vijana katika maeneo mbali mbali Nchini Taasisi hizo zimebuni mradi huo kwa kuwakusanya pamoja vijana ili kuwapatia mafunzo yanayowawezesha kujiepuisha na makundi maovu.

Naye Mratibu wa Mradi wa mafunzo hayo wa Jumuiya ya kupambana na changamoto na kuwaendeleza Vijana Zanzibar { ZAFAYCO } Nd. Abdi Hamid Abeid alisema Jamii inaweza kupunguza uchafuzi wa mazingira endapo itakijika katika katumizi zaidi ya Kompyuta.

Alisema Wanafunzi wa Skuli za Sekondari na Vyuo Vikuu hivi sasa wamekuwa wakitumia kumbu kumbu za vitabu na baadhi ya maandisi na machapisho kupitia mtandao huo badala ya mfumo wa zamani wa kutumia vitabu vilivyokuwa vikitengenezwa kwa karatasi zinazotokana na kukatwa kwa miti.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment