Wednesday, March 4, 2015

WAFANYAKAZI WA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR WAPEWA MAFUNZO JINSI YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA

Mshauri wa mambo ya Afya kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) Dk. Andemichael Ghirmay akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort na yamezaminiwa na WHO.
Mgeni rasmin Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed Jidawi akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mgeni rasmin Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed Jidawi (hayupo pichani) wakati alipokua akifungua mafunzo hayo huko Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mjini Unguja.
Mmoja wawakufunzi kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) anaefanyia kazi Tanzania Dk. Grace Saguti akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha mada yake.
Mgeni rasmin Dkt. Jidawi katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment