Monday, January 5, 2015

TPDC yatumia Dola za Kimarekani Bilioni 1.225 kwa ajili ya mradi wa bomba la gesi

 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Michael Mwande akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzungumzia mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 94.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC),James Andilile akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzungumzia mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 94. wengine pichani ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Michael Mwande (katikati) na Kaimu Meneja Mkuu wa GASCO,Kapwalya Mhisomba (kushoto).
 Sehemu ya Waandishi wa Habari waliofika kwenye Mkutano huo.Picha na Emmanuel Massaka.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) limetumia Dola za Kimarekani Bilioni 1.225 kwa ajili ya mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 94.

Fedha za mradi wa gesi asilia ulitokana na mkopo na mkandarasi ameshalipwa asilimia 81 ya ujenzi wa bomba hilo.

Akizungumza na waandishi habari jana Kaimu Meneja Mkuu wa GASCO,Kapwalya Mhisomba alisema mradi wa bomba la gesi alisema ukikamilika utapunguza gharama za utumiaji wa mafuta katika kuendeshea mitambo ya umeme.

Mhisomba alisema mradi wa bomba la gesi ndiyo hiyo iliyopitisha na hakuna ongezeko lingine liloweza kuongezeka katika mradi huo na mlipaji fedha hizo anachukua benki.

“Tukitaka mambo makumbwa yanawezekana kinachohitajika ni ushirikiano tu kwani nchi hii ni ya wote na sio ya watu wengine wanaweza kutufanyia”alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji James Andilile .

Alisema mradi wa bomba la gesi asilia utapokelewa Juni mwaka huu na kuanza kusambaza maeneo mbalimbali kikwazo cha usambaji wa gesi asilia kwa Dar es Salaam ni mipango miji.

Mhisomba alisema kwenye usambazaji kwa matumizi ya nyumbani na wanashirikiana na chuo kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Chuo cha Sayansi na Teknoloji (DIT).

Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC ,Michael Mwande alisema kukamilika kwa bomba la gesi asilia kutasaidia usambazaji wa umeme vijijini katika maeneo mbalimbali.

Mwande alisema TPDC itaendelea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali wananchi mradi huo pamoja na faida zake katika nchi.

No comments:

Post a Comment