Friday, December 26, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA INDIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Rais wa Lions (Host) Club ya Dar es Salaam, Mathew Levi, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya watoto wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa ya moyo iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Beji ya miaka 50 ya Lions Club na Makamu wa Gavana wa Club hiyo, kwa nchi za Tanzania na Uganda, Hyderali Gangji, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo wanaokwenda nchini India kutibiwa. Hafla hiyo ilifanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Hahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Amina Yahya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya hafla fupi ya kuwaaga watoto hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Hyria Ally (miezi 9) Kutoka Zanzibar, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Zulekha Said.
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment