Monday, October 6, 2014

SEMINA YA KAMATA FURSA,JITATHIMINI,JIAMINI,JIONGEZE YAFANYIKA MJINI DODOMA

MKURUGENZI wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba,(wanne kushoto) akiongea na baaddhi ya wakazi wa Dodoma mjini (hawapo pichani) waliohudhuria Semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Royal Village mapema jana,ambapo aliwaeleza wakazi hao namna ya kuwapatia mbinu mbalimbali za kujikwamua kupitia rasilimali zilizopo ndani ya mkoa huo wa Dodoma.
Msemaji kutoka GS1, Pius Mikongoti akiwalezea wakzi wa Dodoma namna ya kunufaika kupitia huduma zitolewazo na GS1, hasa katika mfumo wa kutumia Barcode.
Msanii wa kughani Mashairi Mrisho Mpoto akiwapa historia yake ya mafanikio na namna alivyoweza kutumia fursa hadi kufikia hapo alipo kwa sasa.
Afisa Utekelezaji na mipango wa NSSF Ally Mkulemba akitoa semina kwa wakazi wa Dodoma, huku akiwapa mbinu za kutumia fursa katika kusongesha mafanikio kupitia mikopo mbalimbali itolewayo na Shirika hilo mapema jana ndani ya Ukumbi wa Royal Village.
Mrisho Mpoto akimkabidhi kifaa cha kupimia magari mmoja wa wakazi wa Dodoma Beatrice Chilewa (kulia), muda mfupi baada ya kujishindia moja ya swali lililoulizwa na msemaji wa GS1, Pius Mikongoti, ambalo lilikuwa likimtaka ataje nchi tatu za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotoa Barcode na namba za utambulisho wa nchi hizo, wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Josekazi Auto Garage ambaye ndiye mmiliki wa kifaa hicho cha kupimia magari.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Josekazi Auto Garage, Joseph Mgaya akiwaeleza wakazi wa Dodoma namna alivyotumia fursa na kumpelekea kumiliki kampuni hiyo inayojishugulisha na huduma za kutengeneza A/C za magari na Ndege na namna alivyo wekeza mpaka sasa,ambao amekuwa akitumia vifaa vya kisasa kikwemo kifaa kinachoweza kupima magari yote na kujua matizo kwa haraka.
Washiriki wa semina hiyo ya fursa wakiunga mkono moja ya mada iliyokuwa ikitolewa ukumbini humo.
Baadhi ya wakazi wa Dodoma waliojitokeza kusikiliza mafunzo mbalimbali kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal Village,nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Msanii wa Bongo Fleva Mwasiti Almasi akiwaeleza wakazi wa Dodoma namna alivyotumia Fursa iliyopo kwenye muziki na kufanikiwa kuwekeza baadhi ya mambo kupitia mafao mbalimbali yatolewayo na Shirika la NSSF.
Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal Village,mjini Dodoma hapo jana.
Mmoja wa wanasemina hao akiuliza swali lililotokana na mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na wasemaji mbalimbali wa Semina ya Kamata Fursa muda mfupi kabla ya kumalizika kwa semina hiyo.
Mtangazaji wa Kipindi cha Leo tena, Gea Habib akizungumza jambo kwenye semina ya Kamata Fursa. 
Meza kuu ya watoa mada ya Kamata Fursa wakifuatilia na kusikiliza baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na washiriki wa semina hiyo.
Mmoja wa akina Mama ajishughulishae na shughuli za ujasiliamali katika suala zina la ubunifu wa mavazi,aliyejitambulisha kwa jina moja la Neema,akimkabidhi zawadi ya  shati msanii wa kughani Mrisho Mpoto,alilolibuni mwenyewe.

No comments:

Post a Comment