Monday, October 6, 2014

Airtel yazindua Mashindano ya kuvumbua vipaji vya Muziki

Mkurugenzi wa kitengo cha Masoko wa Airtel Levi Nyakundi akiongea wakati wa uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama " Airtel TRACE Music Star" kwa lengo la kukuza na kuvumbua vipaji vya wana muziki chipukizi na kuwawezesha kufikia ndoto zao. Program hii ni kwa ushirikiano kati ya Airtel, kampuni ya Trace pamoja na Mwanamuziki wa Marekani Akon, uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa high spirit - IT Plaza jijini Dar es saalam.

Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akiongea wakati wa Uzinduzi wa program ya Airtel Trace Music Star , program itakayowawezesha wanamuziki chipukizi kuonyesha vipaji vyao vya muziki kwa kupitia simu zao za mkononi.



Mwanamuziki wa Bongo Flava Ommy Dimples akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama " Airtel TRACE Music Star"kwa lengo la kukuza na kuvumbua vipaji vya wana muziki chipukizi na kuwawezesha kufikia ndoto zao. Program hii ni kwa ushirikiano kati ya Airtel, kampuni ya Trace pamoja na Mwanamuziki wa Marekani Akon. uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa high spirit - IT Plaza jijini Dar es saalam
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akifatilia kwa karibu uzinduzi wa program ya kusaka vipaji vya muziki ijulikanayo kama Airtel Trace Music Star.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiwa na msaani wa muziki wa kizazi kipya Lady JD wakati wa uzinduzi wa Airtel Trace Music Star.

Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi Kipya AY (pili kulia) akijadiliana jambo na mtayarishaji wa muziki nchini,Lamar wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama " Airtel TRACE Music Star Program inayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel, kampuni ya Trace pamoja na Mwanamuziki wa Marekani Akon. uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa high spirit - IT Plaza jijini Dar es saalam.wengine pichani ni Mtangazaji maarufu nchini Salama Jabiri pamoja na Blogger Shamim Mwasha.
MC Ephrahim Kibonde akiongoza hafla hiyo.
Wadau wa burudani.
Mazungumzo ya hapa na pale.

Wadau hawa pia walikuwepo kwenye hafla hiyo.
sehemu maalum ya vilaji kwa walaji.

Wanalibeneke wakijadiliana mambo,toka kushoto ni Faustin,Kajuna na Othman.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mashindano ya kusaka vipaji vya muziki kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama Airtel TRACE Music Star kwa lengo la kukuza vipaji vya muziki na kuwawezesha wanamuziki chipukizi wa kitanzania kujulikana katika anga za muziki duniani

Uzinduzi huu umefatia ushirikiano kati ya Airtel na Kampuni Muziki ya TRACE pamoja na mwanamuziki nguli wa Marekani Akon

Mashindano haya mbali na kufanyika nchini Tanzania pia yatashirikisha vijana kutoka nchi 13 barani Afrika ambazo Airtel inafanya biashara zake, nchi hizo ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, The Democratic Republic of Congo (DRC), na Gabon, ambapo waimbaji bora kutoka kwenye kila nchi watachaguliwa na kuzawadiwa baada ya kuingizwa kwenye mashindano yatakayowashirikisha waimbaji bora kutoka nchi nyingine ili kupata mshindi atakayetwaa taji la Mwanamuziki mwenye kipaji bora Afrika. Mshindi wa Afrika atajishindia zawadi mbalimbali ikiwemo kurekodi na kusambaziwa nyimbo zake chini ya studio kubwa ulimwenguni pamoja na kufaidika na mafunzo ya kufuliwa kimuziki na Nguli wa Muziki wa Amerika Akon.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa program hiyo Mkurugenzi wa Masoko bwana Levi Nyakundi alisema” mpango huu unaenda sambamba na dhamira yetu wa kuwawezesha vijana wenye ndoto ya kuwa wanamuziki bora kuonyesha uwezo wao kuwawezesha kufikia ndoto zao. Tunafahamu kuwa Tanzania ina vijana wengi wenye vipaji vya muziki lakini bado hawajajulikana katika anga za muziki na ndio maana leo tunazindua program hii na kuwawezesha kujiunga kirahisi kupitia simu yake ya mkononi na kushirikia Airtel Trace Music Stars na kuibuka kuwa wanamziki bora”.

Mashindano haya yatakayoenda kwa muda wa mienzi sita yanaanza kuanzia rasmi hapa nchini siku octoba 7 2014 ambapo mshiriki yeyote atakayependa kushiriki atatakiwa kupiga 0901002233, na kuimba nyimbo zake kwa kutumia simu yake na kutuma kwenye namba hii, kisha nyimbo zake zitasikilizwa na kuchagulia kufudhu kuingia kwenye kinyanganyiro na kuweza kupigiwa kura kuibuka kuwa mwimbaji nyota wa Tanzania na baadae kuwa super star wa Afrika kwa ujumla.

Halikadhalika mashabiki na wapenzi wa muziki wataweza kumpigia kura mshiriki wanayempenda ili kumuwezeshwa nyimbo zake kushinda, ili kumpigia kura mshiriki wako tuma namba/code ambayo mshiriki ataitangaza pindi nyimbo yake itakapochaguliwa kuingia kwenye mashindano au unaweza kuipata wewe mwenyewe kwenye tovuti www.tracemusicstar.com’’Aliongeza Nyakundi.

Akiongea kuhusu program hiyo Mwanamuziki wa Bongo Flava Ommy Dimples alisema’ kwa hakika haya ni mashindano ya pekee yanayotoa fulsa kwa mwanamziki yeyote ambaye angependa kuwa superstar kushiriki.

Napenda kuwahamasisha vijana kuchangamkia fulsa hii kwa kurekodi freestyle yako ya flave yoyote kali kupitia simu yako na kutuma nyimbo yako. Pia napenda kuwaomba mashabiki na wapenzi wa muziki kuwapigia kura washiriki hawa kwa wingi ili kuweza kumpata ushindi. kwa wanamuziki chipukizi mashindano haya si yakukosa maana wewe pia unaweza kuibuka kuwa superstar wa Airtel Trace Music Star kwa njia rahisi tu Piga, Imba, Shinda. aliongeza Dimples.

Airtel imeingia mkataba wa ushirikiano na Trace Music kwa muda wa miaka mitatu ambapo Fainali ya mashindano haya ya Airtel Trace Music 2014 yanategemea kufanyika Mwezi March 2015.

Zawadi nyingine zitakazotoliwa kwa washindi wa mashindano haya ni pamoja na pesa taslimu na simu za mkononi

No comments:

Post a Comment