Thursday, July 17, 2014

HONGERA SANA MR. PRESIDENT 'JAKAYA M. KIKWETE"

Hongera sana Mr. President ‘Jakaya M. KIKWETE’ 

“I am Moved”, sababu nikirudi nyuma kidogo katika historia ya nchi ya Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati sanaa ya muziki wa kizazi kipya ilipoanza kuchipuka ikifuatiwa na vita kubwa dhidi ya kukemea kijana kuwa msanii waHIP HOP nchini na sanaa hii kupewa majina ya kutisha kama muziki wa “kufoka foka, kihuni”na sanaa hii haikukubalika kabisa katika jamii ya kitanzania.
Binafsi naweza nikasema kipindi cha awamu ya 4 ya uongozi wa serikali ya Tanzania kupitia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ‘Dk. Jakaya Mrisho Kikwete’ ndio wakati pekee ambapo wasanii na sanaa ya kitanzania inaweza kujivunia sana. Kwanza kabisa naweza kudiliki kusema ndio wakati pekee wasanii wa nchini wameweza kutembelea IKULU ya Tanzania kuliko vipindi vyote vilivyopita na pia kuwa ni kiongozi ambae amekua na ukaribu wa hali ya juu na wasanii wa nchini. Hata mimi binafsi ambae sijawahi kupata nafasi ya kuingia IKULU, natamani ningekua msanii kipindi hichi ili niweze kupata nafasi ya kuwa na ukaribu na Rais wa nchi yangu na naamini inaleta msukumo mkubwa sana kwa vijana ambao wanafanya sanaa nchini Tanzania kwa sasa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanza tu naweza nikasema dhana ya upendo wa sanaa hii ya Tanzania hajaanza nayo jana wala juzi, sababu kipindi cha nyuma wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alikuwa mstari wa mbele kusikiliza sana muziki wa bongo na alikua anahakikisha anakwenda nao kwa jinsi unavyozidi kukua. 
Rais Kikwete sehemu yake kubwa nakumbuka alikua anahakikisha anapata nyimbo mpya za bongoflava zikitoka ilikuwa ni katika kituo cha Radio cha Clouds FM wakati huo ofisi za radio hiyo zilikuwa pale katika jengo la Kitega Uchumi Samora Avenue. Juhudi za kiongozi huyu wa ngazi ya juu kabisa nchini hazijaishia hapo hata baada ya kuingia madarakani bado tunaziona kwa mialiko kadha wa kadha anayoitoa kwa wasanii kuweza kuingia Ikulu na kupata nao chakula, pia kuzungumza nao na kuwasikiliza matatizo yao ya kimaisha pamoja na kisanii. ukiwa kiongozi wa ngazi za juu katika nchi yoyote majukumu yako ni makubwa sana na ni ngumu kutatua matatizo ya kila mwananchi na kila sekta lakini kuweza kutafuta muda wa kuweza kukutana kuongea nao na kuwasikiliza tu ni kitu mabacho hakijawahi kitokea kwa viogozi wote wa kiserikali waliopita.

 
Si hapo tu Mheshimiwa Rais ameweza kutumia nguvu na juhudi zake kuweza kuwaletea wasanii studio inayoeleweka nchini ili waweze kutengeneza muziki na audio recording zenye viwango vya kimataifa pamoja na malalamiko ya hapa na pale kuwa studio hiyo haijulikani ilipo na inafanya nini hivi sasa lakini hayo sio makosa yake na sidhani kama yanamuhusu, mheshimiwa ameweza kuwapatia kitu hicho na ameendelea na harakati zake kusaidia sanaa hivyo, sitegemei yeye ndio akae kusimamia kuendesha shughuli hiyo wakati ana mambo lukuki na matatizo ya wananchi wengine ya kutatua.

Mbali na hiyo tumeona msaada wake binafsi ambao aliutoa kuweza kumsaidia msanii Ray Cee ambae alikua ameharibikiwa kwa utumiaji wa madawa ya kulevya, aliweza kumsaidia na hivi sasa amerudi katika hali salama na kuweza kuendelea kufanya harakati zake za kisanii na kusaidia vijana wengine kuondokana na utumiaji wa madawa ya kulevya katika Foundation yake ijulikanayo kama Ray C Foundation. 

Juzi tu akiwa nchini Marekani, tumeona alifanikiwa kumkutanisha msanii Diamond Platnumz na mtaalam wa ngazi ya Juu wa muziki wa nchini Marekani ambae anasimamia wasanii kama “Trey Songz na Big Sean ajulikanae kwa jina “Mr Kevin Liles”, huko Manhattan New York City ili aweze kumsaidia msanii huyo ambae amefika hadhi ya kimataifa na kuweza kuwa nominated kwenye tuzo kubwa sana za muziki Duniani kama MTV pamoja na BET na wasanii wengine wa Tanzania ambao wanachipukia katika tasnia ya muziki.

Rais Kikwete hakuishia hapo, aliahidi kuleta na kusaidia tasnia ya muziki na Filamu nchini na amedhihirisha wazi kuwa hajachoka kwa kuweza kufanikisha kuleta wasanii wakubwa sana toka nchini Marekani ambao wapo nchini Tanzania kwa sasa ambao wanafanya Workshop inayoendela katika kumbi za Bank Of Tanzania hivi sasa kwa ajili ya wasanii nchini kupata elimu zaidi ya kazi zao kisanii wanazofanya. Mheshimiwa Rais amefanikiwa kuwaleta Hip Hop Legend Rapper/Producer/Actor/ DAVID BANNER msanii toka MISSISSIPI USA ambae ameshaweka historia kubwa sana katika tasnia ya filamu pamoja na muziki wa Hip Hop ambae yupo nchini pamoja na TERRENCE J ambae alikuwa mtangazaji wa TV kwenye kipindi maarufu sana ndani ya BET ambapo nafasi yake imechukuliwa na msanii aliebadilisha jina lake hivi karibuni kwa mara ya pili kutoka Lil’ BOW BOW alilopatiwa na msaniiSNOOP DOGG wakati akiwa mdogo na kwenda BOW BOW alipokuwa mkubwa na juzi tu amebadilisha tena na anajulikana kwa jina lake halisi SHAD MOSS ambae anafanya kipindi kijulikanacho kama 106 & PARK. TERRENCE J ambae kwa sasa ameingia kwenye tasnia ya Filamu na kushiriki filamu ambayo ni maarufu sana na mastaa wengi nchini marekani “THINK LIKE A MAN TOO” ambayo inaangaliwa sana na ipo katika cinema duniani kwa sasa, iliyotokana na kitabu kilichoandikwa na Legendary comedian“STEVE HARVEY” na hii ni filamu ya 2 kutoka ambayo inetengenezwa kutokana na kitabu hicho.
 
Sanaa ni kitu ambacho huingizia kipato kikubwa sana cha kodi katika serikali za nchi zilizoendelea kutokana na usimamizi mzuri ambao serikali za nchi hizo zimeweza kutengeneza mfumo wa kuweza kuwalinda wasanii pamoja kusimamia haki za kazi zao, vile vile hutengeneza ajira nyingi sana kwa vijana wenye vipaji vya sanaa kuweza kutumia sanaa hiyo kujitengenezea maisha zaidi ya kusubiri mpaka wakaajiriwe. Sanaa hii ya msanii mmoja kwa mfano kama ALIKIBA, OMMY DIMPOZ, DIAMOND Platnumz au LADY JAY DEE ambao wana mafanikio makubwa sana katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, wameweza kusababisha vijana wengi kupata ajira kama wale wanaocheza kwenye show zao (Dancers), watengeneza muziki wao (Producers), wasimamizi wa kazi zao (Managers), mtengeneza Video (Video Director) na wengine wengi, ambapo swala la ajira tunalijua lilivyokuwa gumu nchini na duniani kwa ujumla.
Tunaelewa kabisa kuwa kiongozi wetu huyu amebakiza muda mfupi sana madarakani lakini kwa nguvu hii ambayo ameionyesha mpaka sasa sidhani kama ataishia hapo hata kama akiwa hayupo madarakani. Namuombea heri na afya njema aweze kuendeleza mchakato huu ambao ameufanya mpaka sasa katika sanaa ya Tanzania, mungu ampe nguvu asichoke sababu naamimi wasanii wote nchini tupo nyuma yake kuendeleza legacy ambayo ameianza, vile vile viongozi wengine na kiongozi wa nchi anaekuja baada ya yeye aweze kusaidia kufungua milango na kumsaidia zaidi Baba wa Wasanii nchini Dk JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa moyo wake na msukumo wa kusaidia sanaa nchini alioanza nayo zaidi ya miaka 10 iliyopita na mimi binafsi nikiwa kama shahidi kwa makubwa aliyoyafanya mpaka hivi sasa.

Hongera mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ‘Dk. Jakaya Mrisho Kikwete’ kwa kazi yako nzuri ya kusaidia sanaa nchini Tanzania na Mungu akubariki sana.

By: GongaCEO

No comments:

Post a Comment