Monday, June 2, 2014

SPORTS XTRA DAY YAFANA JIJINI ARUSHA

Zenith Media Yatwaa Kombe la Sports Extra Day Bonanza kwa Jiji la Arusha.
Timu ya Banana investiments ikisali kabla ya kuanza kwa mchezo.
Huyu nae alikuwa aki #BRAZUCA katika mchezo wa Sports Xtra Day Jijini Arusha.
Mbwiga wa Mbwiguke the Captain wa Sports Xtra akiwapanga vijana wake.
Huyu kijana nae alipata wasaa wa kuongea na Shaffih Dauda kuwa ana kipaji cha utangazaji wa mpira ,sasa atafikaje hapo yeye (Shaffih) alipo?
Super Striker Shaffih Dauda wa Sports Xtra akichomoka na mpira katika bonanza la Sports Xtra Day ndani ya Sheikh Amri Abeid ,Jijini Arusha.
Captaiiiiiiiiin wa Sports Xtra Mbwiga Mbwiguke akielekea mapumziko na wenzake, pamoja na kucheza pia alitoa burudani sana kwa mashabiki na watazamaji wa Sports Xtra Day Bonanza.
Hapa ni timu ya Mega Trade investments (K-Vant) wakicheza na Kitambi Noma.

Muonekano mzuri wa uwanja wa kumbu kumbu ya Sheikh Amri Abeid na mlima Meru.
Wadhamini wa Sports Xtra Day ni Clouds Media Group, Mega Trade Investments (K -Vant), Banana Investments, SBC Company Limited (Pepsi) ,Zenith Media na Wazalendo 25 Blog.
Timu ya Zenith Media wakipanga mashambulizi yao
Mshindi wa pili ni Timu ya Makocha wa Arusha wakitoka na Kombe lao.
Mkurugenzi wa mauzo na Masoko wa MegaTrade Investments (K -Vant) Bw. Good Luck Kway akiongea machache, pamoja na kuipongeza Clouds Media Group na kuitaka waongeze makampuni mengine na mashindano yawe ya siku tatu au hata wiki nzima.
Mwakilishi toka Banana Investments akizungumza machache kuhusu shindano la Sports Xtra Day
Mwakilishi wa Zenith Media akiwashukuru waandaji wa Sports Xtra Day na kufurahia kwa Ushindi walioupata.
Cameraman toka Clouds Media Group Ezra Kaaya akifanya yake katika Sports Xtra Day ,jijini Arusha.
Shaffih Dauda akipata picha na Shabiki wa Kitambi Noma
Wazee wa Kitambiiiiiii Noooma.....wakifurahia kwa ushindi wa Raundi ya kwanza

Mbwiga wa Mbwiguke the Captain akipata Picha na Mashabiki wa Kitambi Noma, Kulia mwenye Box ya huduma ya kwanza ni Jimmy Chocolate 'Mukate'

Mchezaji wa zamani wa AFC na Zingine Muhidin Cheupe akisalimiana na Mbwiga Mbwiguke
Mbwiga wa Mbwiguke na shabiki wa Kitambi Noma



Mchezaji Bora ni Abuu Juma wa Timu ya Makocha wa Arusha na anaichezea mtibwa ya Morogoro akipata chupa moja ya K- Vant toka Mega Trade Investment


Na Gadiola Emanuel wa Wazalendo 25 Blog - Arusha



Timu ya Zenith Media imeibuka mshindi wa Sports Extra Day Bonanza kwa kuifunga timu ya Makocha wa Arusha kwa njia ya penati baada ya kutoka sare bila ya kufungana, iliyofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Michuano hiyo ilishirikisha timu nane na kupelekea timu ya Sports Extra kutolewa kwa hatua ya mtoano, huku nahodha wake Mbwiga Mbwiguke akishindwa kuendesha timu vema ila kuambulia kuleta burudani kwa mashabiki katika mchezo huo.

Sports extra Day Bonanza ilishirikisha makampuni tofauti tofauti ya hapa jijini Arusha. Timu hizo ni clouds sports extra , Kitambi noma, Aqua Kings ,na SBC Company inayotengeneza kinywaji cha Pepsi.

Pia zilikuwepo timu ya Zenith Media, Timu ya Makocha wa Arusha, Banana na Mega trade investment (K vant) , ambapo zilicheza kwa hatua ya mtoano, kwa hatua ya kwanza timu ya makocha ilicheza na Aqua kings  na timu ya maocha kuibuka na goli 1 -0 , kitambi noma na Pepsi na timu ya pepsi kuibuka na ushindi wa bao 1- 0, clouds fm na zenith media ambapo zilitoka suluhu bila kufungana, na  Mega Trade Investiments (K-Vant) na Banana pia zilitoka suluhu bila kufungana .

Hatua ya pili ilicheza kitambi noma na K-vant  ambapo kitambi noma iliibuka na goli 1- 0 dhidi ya Mega trade investiment, zenith media ilicheza na timu ya makocha ambapo walitoka 1-1. pia clouds fm ikacheza na Aqua zilitoka suluhu bila kufungana huku pepsi ikiifunga timu ya Banana Investiment.

Timu nne zilizoingia nusu fainali ni timu ya Makocha wa Arusha na kitambi noma ambapo kitambi noma ilibamizwa 2 -0 , huku Zenith Media ikiibamiza timu ya Pepsi kwa goli 1-0 na kutinga fainali. Timu ya Arusha na Zenith Media ziliiingia Fainali.

Mwakilishi wa TFF kwa mkoa wa Arusha Bw. Omari Wali aliwapongeza Clouds Media Group kwa kuanzisha mashindano hayo ila ikawaasa washirikishe makampuni mengine yalipo hapa Arusha. Picha zote na Gadiola Emanuel wa Wazalendo 25 Blog

No comments:

Post a Comment