Sunday, June 8, 2014

MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD NDIO MAZIWA BORA TANZANIA YASHINDA TUZO YA UBORA KWA MIAKA MIWILI MFULULIZO ,MAKAMPUNI 30 YAACHWA MBALI

Afisa masoko wa kampuni ya maziwa ya Asas  Dairies Ltd ya mkoani Iringa Bw Jimy Kiwelu akitoa maelekezo ya kwanini maziwa ya Asas ni  bora  kuliko  maziwa mengine nchini
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani,kulia akimpongeza afisa masoko wa kampuni ya Asas  Dairies Ltd Bw Jimmy Kiwelu baada ya kampuni  hiyo kushinda tuzo kwa mara nyingine ya uzalishaji bora wa maziwa nchini Tanzani na kuzibagwa kampuni mbali mbali hapa nchini
Banda  la maonyesha la kampuni ya Asas  Dairies Ltd
Afisa masoko wa kampuni ya maziwa ya Asas  Dairies Ltd ya mkoani Iringa Bw Jimy Kiwelu akishangilia baada ya  kampuni yake  kuwa ndio kampuni  bora ya uzalishaji maziwa nchini Tanzania katika mashindano yaliyofanyika mkoani mara
Watoto  wa mkoa wa Mara  wakishangaa ubora wa maziwa ya Asas kutoka Iringa
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani kulia na  viongozi  wengine wakifuatilia maonyesho hayo huku  wakifurahia ubora wa maziwa ya Asas Dairies Ltd




ambao ni mabingwa
Na Francis Godwin Blog
KAMPUNI ya maziwa ya Asas Dairies Ltd ya  mkoani Iringa kwa mara ya  pili mfululizo imefanikiwa  kuongoza kwa  ubora  wa  uzalishaji wa maziwa baada ya  kukabidhiwa  tuzo ya mshindi wa kwanza kwa  viwanda vya maziwa bora nchini Tanzania kwa  kuzibwaga vibaya kampuni   30 zilizoshiriki.

Asas Dairies  Ltd  yenye makao yake makuu mkoani Iringa imekabidhiwa tuzo ya ushindi wa kwanza kwa mwaka 2014 katika viwanda bora  vya maziwa  katika maonyesho ya wiki ya maziwa yaliyofanyika  mkoani Mara ambapo mgeni rasmi alikuwa ni  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani.


Akiipongeza kampuni  hiyo ya Asas Dairies  Ltd  kwa  kuendelea  kufanya  vizuri katika mashindano hayo ya ubora  wa maziwa nchini  ,waziri Dr Kamani  alisema  kuwa jitihada  zilizoonyeshwa na kampuni  hiyo ni kubwa na  zinapaswa  kuigwa na makampuni mengine hapa nchini.

Kwani  alisema  kuwa  kuongoza katika nafasi zote zilizoshindaniwa na jambo dogo ni  jitihada  kubwa zimefanyika na ni hatua ya kujivunia kwa kampuni hiyo.

Pia  alisema kwa   aliipongeza  bodi ya maziwa Tanzania kwa  kuandaa mashindano kama hayo kwani ni sehemu ya  kipimo kwa  wamiliki wa  viwanda vya maziwa  nchini kujitathimini .

Kwa upande  wake afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Jimmy Kiwelu  alisema kuwa mbali ya kampuni  hiyo kuongoza kwa mwaka  huu bado  ilipata  kuongoza katika mashinadano kama haya  yaliyofanyika mwaka jana mkoani Ruvuma na  kuwa lengo la kampuni ni kuendelea  kuongoza  daima 

Katika mashindano hayo  yaliyoandaliwa na bodi ya maziwa  Tanzania( TDB) jumla ya makampuni 30 yalishiriki  ikiwemo kampuni ya Tanga fresh,Musoma Dairies,Kilimanjaro creamer,Engingten,Arusha,Ammy Dairies Njombe cefa,Victoria dairies ,Uvingo dairies na mengine mengi kampuni ya Asas Dairies iliweza  kuibuka na ushindi  wa  jumla baada ya kushinda tuzo zote  tatu  zilizokuwa  zikishindaniwa na hivyo kufanikiwa  kuondoka na tuzo nne  zote ikiwemo ya mshindi wa  jumla.

 Kiwelu  aliwataka  watanzania kuendelea  kuzipenda  bidhaa za Asas Dairies Ltd  kutokana na kuendelea kuongoza katika ubora na kuwa lengo  la kampuni hiyo ni kuona ubora  huo unaendelea zaidi na kila mwaka kuendelea  kufanya vema.

Pia  alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa  wanaoutoa kwa  kuendelea  kutumia maziwa yanayozalishwa na kampuni  hiyo ya Asas Dairies Ltd Iringa.

No comments:

Post a Comment