Sunday, June 8, 2014

KONGAMANO LA MAJI LAFANYIKA JIJINI DAR

Wiki hii jijini Dar es salaam kumefanyika Kongamano kubwa la wadau wa maji kutoka kila kona ya nchi hii. kubwa lililofanyiwa kazi na wataalam hao wa maji ni kujulishwa teknolojia mpya ya mabomba iliyokuwa inatambulishwa na kampuni kubwa ya teknolojia ya mambomba ya Borouge kutoka Falme za Kiarabu. 

Borouge ilileta wataalam wanne ambao ni Mario Andrade, Farraj Tashman, Andrew Wedgner na Reda Ashkar. walionufaika na mafunzo hayo ni waliotoka Mamlaka za Maji mijini na vijiji, Wahandisi, Washauri katika fani zote za maji, ujenzi na gesi. 

pia washiriki walifahamishwa kuwa sasa lile tatizo la mabomba ya matumizi yote yamefika mwisho kwani kiwanda cha pipe industries cha vingunguti mjini dar es salaam kitakidhi mahitaji ya nchi nzima na kuwa na ziada ya kuuza nje kwa amabomba ya aina zote kama vile hdpe, pvc, grp na mabomba chuma kwa upenyo wa 60mm mpaka zaidi ya 3,200mm. 

Mgeni Rasmi katika kongamano hilo alikuwa Waziri wa Maji,Professor Jumanne Maghembe ambaye alionyeshwa kufurahishwa kwake na uwepo wa kiwanda kama hicho ambacho kinamilikiwa na wazawa kinahesabika kama kikubwa kuliko vyote afrika mashariki na kati pia cha aina yake kwa kuweza kuwa na uzalishaji wa mabomba aina yote katika kiwanda kimoja na chenye uwezo wa kuajiri watu 500.
Waziri wa Maji Professor Jumanne Maghembe (kulia) akikagua bidhaa za mabomba yanayozalishwa na kiwanda cha Pipe Industries cha mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la wataaalam wa maji lilifanyika hivi karibuni. wa pili kushoto ni Mwekezaji Mzawa wa Kiwanda hicho Bwana Nassor Ally Seif.
Mwekezaji Mzawa wa Kiwanda cha Pipe Industries Bwana Nassor Seif (kushoto) akimsikiliza Waziri wa Maji Professor Jumanne Maghembe akimweleza jambo kuhusiana na mabomba yanayozalishwa na pipe industries wakati akikagua maonyesho ya kiwanda hicho katika kongamano la maji lilofanyika mjini dar es salaam.
Waziri Mageembe akizungumza na waandishi wa habari baaada ya kufungua kongamano la maji.
Waziri wa Maji Professor Jumanne Maghembe (wa pili kutoka kushosto) akifurahia jambo na wamiliki wa pipe industries bwana nassor seif (kushoto) na seif seif (wa pili kulia) wakiwa na baadhi ya washiriki wa kongamano la maji. kulia ni bibi esther baruti kroll mwakilishi mkazi wa kampuni ya saruji ya dangote industries.
wataalam vijana wa tanzania ni miongoni mwa washiriki na wawezeshaji wa kongamano la maji. kushoto ni moses nkanda bingwa katika mambo ya mabomba ya gesi na mtaalam mshauri bwana subiro mwapinga.
Mtoa Mada katika Kongamano la Teknolojia ya Maji kutoka Kampuni ya Borouge,Bwana Mario Andrade akitoa maelezo kwa washiriki wa kongamano la maji juu ya borouge na uwezo wake katikasekta ya mabomba.
washiriki wakifuatilia kongamano.
Mkurugenzi wa Superdoll,Bwana Jamal Bayser (kulia) na Mkurugenzi wa Reni International,Bwana Dipak Vassa.
Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Mabomba cha Pipe Industries,Bwana Sebastian Kyoni (kulia) akiwa na wataalam wenzake wakishiriki katika kongamano la maji jijini dar es salaam.
waziri wa maji professor jumanne maghembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano la maji.
meneja wa super star forwarders bwana fulgence bube (wa pili kulia) akielezea jambo kwa washiriki wenzake wa kongamano la maji. wa pili kushoto ni mkurugenzi wa superdoll bwana jamal bayser.
Bwana Andrew Wedgner wa Kampuni ya Borouge ya falme za kiarabu akitoa utalaam wake juu ya mabomba ya pe 100 wakayi wa kongamano la maji lilokuwa linafanyika mjini dar es salaam. kushoto ni bwana reda ashkar ambaye amebobea katika uunganishaji wa mabomba ya hdpe na ufundishaji wa teknolojia hiyo btoka kampuni ya borouge.
Mkurugenzi Mtendaji wa Pipe Industries Bwana Seif Ally Seif akitoa maelezo ya kiwanda chake katika kongamano la maji lilofanyika jijini dar es salaam.

No comments:

Post a Comment