"Niliamini kuwa itatuchukuwa muda mrefu kusafiri kuweza kujenga na kutengeneza kitu ambacho kitatambulika kitaifa kitakuwa na heshima inayostahili na kitatoa mchango unaostahili na kitashawishi wachimbaji wengine kuona kwamba hii ni Fursa ambayo hakuna yeyote yule anayeweza kuiacha ipite pembeni. Sasa wacha niwapongeze NSSF kwa kuwa wajanja kati ya mifuko mingine yote ya jamii na kuamua kuliangalia kundi hili ambalo nguvu yake ya baadaye italiongoza taifa kuwa na matajiri wake wa ndani nikimaanisha wawekezaji wa ndani wenye nguvu Mabilionea" alisema Naibu Waziri wa Nishati na Madini Steven Masele.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa
Shirika la taifa la Hifadhi ya jamii NSSF Crescentius Magori akizungumza wakati
wa semina iliyoandaliwa na NSSF kuhusu mfuko huo kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza..
|
No comments:
Post a Comment