Balozi
wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa
Mataifa, Geneva, Mhe. Modest Mero, akimkaribisha Balozi wa Jamhuri
ya watu wa China-Geneva, Liu Jieyi katika tafrija maalum ya maadhimisho
ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika katika
ukumbi wa
ILO hii leo na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali ikiwemo
balozi huyo China UN mjini Geneva, Balozi wa Kenya, Balozi wa Afrika
Kusini,
Balozi wa Togo, Balozi wa Botswana, Balozi wa Cameroon, Balozi wa
Rwanda, wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na
Watanzania
waishio Switzerland. Kushoto ni Mke wa balozi huyo Rose Mero.
Mke
wa Balozi Mero, Rose Mero akisalimiana na ujumbe wa Ubalozi wa
Denmark. pamoja nao ni Balozi Modest Mero na Balozi wa Dernmark-UN.
Balozi Mero akijumuika na mabalozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria katika tafrija hiyo.
Familia ya Balozi Mero katika picha ya Pamoja.
Wanawake mbalimbali waliohudhuria tafrija hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mke wa Balozi Mero.
Balozi
Mero alitoa hotuba ambayo ilielezea
historia, maendeleo, na maendeleo ya mchakato wa Katiba mpya, Hotuba
hiyo pia iliweza kubaiinisha wazi ni vipi Tanzania na Watanzania
wameweza kumudu kurumu katika muungano huo kwa miaka 50 sasa.
Afisa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania UN, Hamisa Mkoma akiwa na Mke wa Balozi wa Tanzania UN, Mama Rose Mero
Afisa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania UN, Hamisa Mkoma akiwa na Mke wa Balozi wa Tanzania UN, Mama Rose Mero
Balozi Modest Mero akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa katika Ubalozi wa Tanzania UN mjini Geneva.
Wageni mbalimbali waliohudhuria tafrija hiyo.
No comments:
Post a Comment