Friday, December 13, 2013

Mhe. Ndugai akerwa na unyanyasaji wa wakulima unaofanywa na watendaji kutoka wilaya ya kiteto pamoja na kufumbia macho wafugaji

Mbunge wa jimbo la Kongwa mkoani Dodoma, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, akihutubia mamia ya wakulima huko Kibaigwa mkoani humo Jumatano Desemba 11, 2013. Ndugai akiwakilisha wabunge kutoka majimbo ya mkoani humo yanayopakana na wilaya ya Kiteto, mkoani manyara, wamekemea vikali uamuzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, kuwafukuza wakulima kutoka nje ya wilaya ya Kiteto na kuwakumbatia Wafugaji kuendelea na wa kimasai kuendelea na shughuli za uchungaji wa mifugo na kufananisha kitendo hicho ni sawa na ubaguzi.
Mbunge wa Kondoa Kusini Mkoani Dodoma aliyekuwa ameambatana na Naibu Spika Mhe. Juma Nkamia akiwahutubia wakulima hao katika Mji wa Kibaigwa na kuwahakikishia kuwa watafikisha kero zao kwa Mhe. Waziri Mkuu ili kupata ufumbuzi wa tatizo la kufukuzwa kwa wakulima hao katika maeneo yao huko Kiteto.
Mhe. Richard kapinye Diwani wa Kata ya Kibaigwa akieleza kwa hisia kali baadhi ya kero zinazowakabili wakulima hao kutokana na kunyanyaswa na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kuwafukuza katika maeneo yao na kufumbia macho vitendo vya wafugaji kuwaua wakulima na hakuna hatua zinazochukuliwa.
Baadhi ya wakulima wakimweleza Mbunge wa jimbo la Kongwa mkoani Dodoma, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai baadhi ya matukio ya kunyanyaswa na Watendaji wa Wilaya ya kiteto na vitendo vya wafugaji kuwafanyia vurugu mara kwa mara katika mashamba yao. Picha zote kwa hisani ya Bunge.

No comments:

Post a Comment