Saturday, December 14, 2013

Mfuko wa Pensheni wa LAPF Wafanya Kufuru Tuzo za NBAA, Watwaa Tuzo ya Kwanza, Mara Tano Mfulululizo

Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Mkazi, Mhe. Goodluck Ole Medeye, akikabithi tuzo ya mshindi wa kwanza ya hesabu bora za mwaka 2012 katika sekta ya hifadhi ya jamii iliyochukuliwa na Mfuko wa Pensheni wa LEPF ambapo ilipokelewa na Mkurugenzi wa Fedha wa Lapf, John Kida. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno. Sherehe hizo zimefanyika jana usiku katika hoteli ya Naura Springs mjini Arusha.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, John Kida, mwenye tuzo, akionyesha Tuzo ya Ubora wa mahesabu kwa wafanyakazi wa LAPF mara baada ya kukabidhiwa. Kutoka Kushoto ni Mhasibu Mkuu wa LEPF, Rock Massawe, Meneja Kanda ya Kaskazini, Rajab Kinande, na kulia ni mtumishi wa LEPF Arusha, Flowin Ngonyani wakati wa sherehe za kukabidhiwa tuzo za NBAA zilizofanyika jana usiku katika hoteli ya Naura springs, Arusha.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, John Kida, mwenye tuzo, akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya NBAA ya ubora wa mahesabu kwa sekta za hifadhi za jamii. Kulia ni Afisa Masoko wa LAPF, Rehema Mkamba na Kushoto ni Mhasibu Mkuu wa LAPF, Rock Masawe wakati wa sherehe za kukabidhiwa tuzo za NBAA zilizofanyika jana usiku katika hoteli ya Naura springs, Arusha.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, John Kida, mwenye tuzo, akipozi na tuzo mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya NBAA ya ubora wa mahesabu kwa sekta za hifadhi za jamii. Kushoto ni Yustino Nyendeza, Rajabu Kinande, Kulia ni Afisa Masoko wa LAPF, Rehema Mkamba na Mhasibu Mkuu wa LAPF, Rock Masawe wakati wa sherehe za kukabidhiwa tuzo za NBAA zilizofanyika jana usiku katika hoteli ya Naura springs, Arusha.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, John Kida, mwenye tuzo, akipongezwa na Afisa Masoko wa LAPF, Rehema Mkamba mara baada Mfuko wa Pensheni wa LAPF kushinda tuzo hiyo wakati wa sherehe za kukabidhiwa tuzo za NBAA zilizofanyika jana usiku katika hoteli ya Naura springs, Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Sekta ya Mifuko ya Hifadhi za Jamii, SSRA, Irene Isaka akiwapongeza watumishi wa LAPF, mara baada ya kushinda kwa Tuzo ya ubora wa mahesabu katika sekta ya Hifadhi za Jamii, Kushoto ni Afisa Masoko wa LAPF, Rehema Mkamba na wa pili Kulia ni Meneja Hazina wa LAPF, Fortune Magambo na Kulia ni Meneja Kanda ya Kaskazini wa LEPF, Rajab Kinande.
Watumishi wa Mfuko wa Pensheni wa LEPF, wakijipongeza kwa Shampeni, mara baada ya Kutwaa Tuzo ya ushindi wa kwanza wa hesabu bora za mwaka 2012 kwa sekta za hifadhi za jamii iliyotolewa na Bodi ya Wahasibu nchini NBAA katika hafla iliyofanyika jana katika Hoteli ya Naura Springs, mjini Arusha.
Watumishi wa Mfuko wa Pensheni wa LEPF, John Kida, Rehema Mkamba, Flown Ngonyani, Elias Mwangingo, Rock Massawe na Rajabu Kinande. wakipozi na tuzo yao, mara baada ya Kutwaa Tuzo ya ushindi wa kwanza wa hesabu bora za mwaka 2012 kwa sekta za hifadhi za jamii iliyotolewa na Bodi ya Wahasibu nchini NBAA katika hafla iliyofanyika jana katika Hoteli ya Naura Springs, mjini Arusha.


Mfuko wa Pensheni wa LAPF, umeibuka tena kuwa ndio Mfuko Kinara wa Tuzo za Bodi ya Uhasibu Nchini, NBAA za Utunzaji Bora wa Mahesabu kuliko mifuko mingine ya Pensheni nchini, kufuatia kushinda tena tuzo hii katika sherehe zilizofanyika jana usiku katika Hoteli ya Naura Springs, hii ikiwa ni kwa mara ya 5 Mfulululizo kwa mfuko huo wa LAPF kushinda tuzo hiyo.

Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Mkurugenzi wa Fedha wa LAPF Bw. John Kida, Amesema LAPF inajisikia fahari sana kushinda tena tuzo hii, hivyo hicho ni moja ya viashiria kuwa sifa za LAPF kama mfuko Bora kabisa wa Pensheni nchini Tanzania, zinatambuliwa na Taasisi mbalimbali.

Akizungumzia sababu za Mfuko wa Pensheni wa LEPF kuwa ndio mfuko pekee wa pensheni, unaoshinda tuzo hiyo mwaka hadi mwaka wakati Tanzania unayo mifuko sita ya pensheni, Bw. Amesema hii ni kufuatia Mfuko wa LEPF kutumia mifumo ya kisasa kabisa ya utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu ya Navision na PMS (Pension Management Systeam) inaowezesha kufunga mahesabu kitaalamu kwa viwango vya kimataifa.

Akiuzungumzia ushindi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Bibi Irene Isaka, amesema Mfuko wa LEPF, umekuwa ukishinda tuzo hiyo mwaka hadi mwaka kutokana na kukosekana kwa muongozo wa utunzaji wa mahesabu, hivyo kila mfuko kuwa huru kutumia mfumo wake wa kimahesabu, hali iliyopelekea LEPF kuibuka kidedea mwaka hadi mwaka, lakini kuanzia sasa, SSRA tayari imeishatoa muongozo kwa mifuko yote kufuata, hivyo kuanzia mwakani, LEPF inapata washindani kwa vigezo vinavyofanana.

Ushindi huu kwa mfuko wa LEPF ni ushindi wa pili kwa mwaka huu, kufuatia mfuko huo huo wa LEPF kutwaa tuzo ya SSRA kama Mfuko unakua kwa kasi zaidi, katika mashindano ya mifuko yote ya hifadhi ya jamii, iliyoitwaa mapema mwaka huu, wakati wa Wiki ya Mifuko ya hifadhi za Jamii nchini iliyofanyika Dodoma, Mwezi Mei Mwaka huu.

Akihutubia Wadau wa LEPF katika Mkutano wake wa Wadau mwezi October mwaka Huu, Mkurugenzi Mkuu wa LEPF, Bw. Eliud Sanga, alisema hii ni mara ya mwisho kwa LEPF kushiriki mashindano hayo, kwa sababu imechoka kujikuta yenyewe ndio inajikuta inashinda kila mara, hivyo kupunguza ari ya ushindani kwa mifuko mingine, ili kutoa furasa kwa mifuko mingine nayo angalau ishinde, itapunzika kwa muda ili kuipa mifuko mingine fursa za kufikia kiwango cha LEPF ili itakapoingia tena, ipate upinzani kujenga ari ya ushindani.

Akizungumzia sifa nyingine za LEPF, Afisa Masoko wa LEPF, Bibi. Rehema Mkamba, amesema LEPF ndio mfuko unaongoza kwa kutoa mafao mengi, ambapo unatoa fao tisa ambayo ni mafao ya uzeeni, mafao ya mirathi, mafao ya kuumia kazini, mafao ya kujitoa, mafao ya uzazi, msaada wa mazishi, mikopo ya nyumba, na mikopo ya wanachama kupitia Saccos.

Bi Mkamba amesema, LEPF ndio inayoongoza kwa mafao bora ya kustaafu, huku pia ukiongoza kwa ulipaji mafao mapema ambapo mstaafu wa LEPF analipwa mafao yake ya kustaafu kabla hata tarehe yake ya kustaafu haijafika.

Bi Mkamba aliongeza, LEPF, ndio mfuko pekee wa pensheni, unaowakopesha wanachama wake mkopo wa kujengea nyumba, ambapo mwanachama anakuwa huru kujenga aina ya nyumba anayoitaka, na katika eneo lolote analotaka na kwa gharama mwanachama atakayoimudu, kinyume cha mifuko mingine inayotoa nyumba zinazofanana na zikiwa katika eneo moja, yaani nyumba za kota.

Mfuko huu wa LEPF, wenye makao yake makuu mkoani Dodoma, umetapakaa katika kanda sita za Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Iringa na Arusha, na ina jumla ya wanachama 102, 187.

Mgeni rasmi katika Tuzo Hizo, ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Goodluck Ole Medeye

No comments:

Post a Comment