Wednesday, December 11, 2013

Mh. Sumaye ahimiza uwekezaji kutoka Uingereza na apokea tuzo la amani na uongozi bora

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amehimiza Waingereza na Watanzania wanaoishi nje ya nchi, kuongeza kiwango cha uwekeza nchini ili kuchangia ukuaji wa uchumi nchini. Aliyasema hayo jana jijini London, Uingereza wakati akihutubia Mkutano wa Biashara na Uwekezaji ulioandaliwa na taasisi ya The New Deal Africa ya nchini humo.

Taasisi hiyo ilishirikiana na Ubalozi wa Tanzania, Kituo cha Biashara cha Tanzania na Kituo cha Biashara na Uwekezaji cha Uingereza (UKTI) kufanikisha mkutano huo.
Balozi Peter Kallaghe akimkabidhi tuzo la amani na uongozi bora Mheshimiwa Fredrick Sumaye.
(TCRA imepewa Award ya Taasisi Inayoboresha Maisha ya Watanzania kwa huduma kwa jamii kwa kusimamia sekta ya Mawasiliano.) Ndugu innocent Mungy akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya TCRA  na Mh.   Sumaye alisema ni matumaini yake kwamba ikiwa Watanzania hao na serikali ya Tanzania, watatumia matokeo ya mkutano huo ipasavyo, watashiriki na kuchangia ukuaji wa pato la taifa. “Ni matumaini yangu kuwa matokeo ya mkutano huu yataongeza miradi ya uwekezaji Tanzania kutoka kwa wawekezaji wa Uingerezana raia wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi,” alisema.
(Jestina Blog kachukua tuzo la Blog safi UK) Alisema awali ilijengeka dhana potofu kwamba raia wanaoishi nje ya nchi, hawana uzalendo na kwamba waliyakimbia mataifa hivyo kukosa hadhi ya kukaribishwa nyumbani wanaporejea. Alisema dhana hiyo imepitwa na wakati na kwamba hivi sasa wamekuwa watu muhimu kwa ujenzi, maendeleo na ustawi wa jamii.
(Said surur akiwakilisha Meru services- DIASPORA ECONOMIC DEVELOPMENT AND POVERTY RELIEFE) Kimsingi, raia wanaoishi nje ya nchi wanajumuisha wafanyakazi katika taasisi mbalimbali, zikiwamo za serikali, wataalamu na wafanyabiashara “Kwa hiyo raia hao wana ujuzi na utaalamu wa kutosha, uwezo wa kibiashara na uzoefu katika matumizi ama kupata rasilimali tofauti,” alisema. Aliwataka Watanzania wanaoishi Uingereza, kuwa mabalozi na washawishi kwa wawekezaji, wakiwaaminisha nchi Tanzania ni mahali bora na salama zao kwa sekta hiyo barani Afrika.
(Mr and Mrs Kassongo wa Kass Grill –Northampton wachukuwa tuzo la’ Jiko’ bora- BEST UK EAST AFRICA GRILL OF THE YEAR 2013) Alizitaka baadhi ya fursa za kibiashara zilizopo nchini kuwa ni mazingira bora ya uwekezaji yanayochagizwa na usalama kwa kibiashara.

Alisema Afrika inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo hatari inayotokana na kuwa mfano wa ‘uwanja wa mapambano’ ya kiuchumi kwa mataifa mengine, hali inayosababisha kutoweka kwa mamlaka ya kimaadili kwa baadhi ya maeneo.
Bi amina ,mjuku wa Shaban Robert achukua tozo kwa niaba ya familia- EDUCATION ADVANCEMENT AWARD 2013 Sumaye alisema `mapambano ya kiuchumi’ kwa mataifa ya nje yanayoendelea Afrika, yanahusu rasilimali zilizopo.
(Dart Foundation wa Nertherland wala tuzo kwa ajili ya kazi zao za kuboresha maisha ya watoto Mwanza Tanzania- WOMEN AND GIRL EMPOWERMENT AWARD 2013)

Alisema kutokana na kasi ya maendeleo na biashara, rasilimali nyingi zinatumika kwenye mataifa mbalimbali duniani. Alisema hatua ya Afrika kutokuwa na uwezo wa kugundua, kuibua na kuzalisha bidhaa zinazotokana na rasilimali za asili, imesababisha mataifa mengi hususani yaliyoendelea kujielekeza barani humo ili kunufaika.

Sumaye alisema mapambano hayo yanashuhudia China ikiingia kwa kasi barani humo, hatua anayohoji kuhusu wanaoihofia nchi hiyo, kati ya Waafrika ama mataifa yaliyowahi kupora rasilimali za barani humo.

“Kwangu mimi, kuingia kwa China kuna manufaa barani Afrika kwa vile sasa kuna ushindani mkubwa unaotoa fursa nyingi iwapo kutakuwa na umakini na kutetea maslahi yetu katika majadiliano ya kibiashara,” alisema. Kwa taarifa zaidi tembelea www.newdealafrica.co.uk.Tel +4474625225043/+447960811614 www.newdealafrica.co.uk

No comments:

Post a Comment