Tuesday, December 10, 2013

MeTL yazindua show ya mwaka kwa watoto na vijana

IMG_9729
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kusaidia jamii kupitia (Corporate Social Responsibility) kama njia mojawapo ya kupiga vita umaskini katika nchi za bara la Afrika. Kushoto kwake ni Meneja Mkuu Ledger Plaza Bahari Beach, Wissem Souifi, Kulia ni Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi na Kushoto ni Irfaan Jaffer kutoka MeTL.
.Lengo la maonyesho ni kusaka vipaji miongoni mwa vijana
.Kuanzia siku ya Krimasi hadi Boxing day zawadi mbalimbali na Tsh m kushindaniwa

Na Damas Makangale

KAMPUNI YA MOHAMMED ENTERPRISES (MeTL) Tanzania kwa kushirikiana Ledger Plaza Bahari Beach wamezindua maonyesho ya elimu ya mwaka kwa watoto nchini yenye kushindaniwa zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla kujinyakulia fedha taslimu Tsh5m.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwenye hoteli ya Ledger Plaze Bahari Beach Hotel, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Bi Fatema Jaffer, amesema kampuni ya Metl ina jail maslahi ya wateja wake na watanzania kwa kupitia dhana ya Kusaidia Jamii na Kujenga mahusiano (Corporate Social Responsibility) kwa kusaidia kuinua vipaji vya watoto.

“Kwenye maonyesho haya ya wazi ya kutazama vipaji mbalimbali vya watoto hasa kwenye elimu tumeamua kudhamini maonyesho haya ili kusaidia jamii kuweza kukuza vipaji vyao vya manufaa yao binafsi na jamii kwa ujumla,” amesema.

Bi. Jaffer amesema kuwa katika taifa la Tanzania kuna vipaji vingi hasa kwa vijana na watoto lakini wanakosa msukumo na jamii kuwatia moyo ili vipaji vile viweze kufanya kazi kwenye jamii na taifa kwa ujumla.

Amesema maonyesho hayo yataanza rasmi kuanzia tarehe 25th, 26 na 27 kwenye viwanja vya Ledger Plaze Bahari Beach yenye dhumuni ya kugundua, kutambua kuendeleza, kutia moyo na kupapanua vipaji vya watoto vilivyojivicha kwenye jamii ya watanzania.
IMG_9735
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho hayo ya watoto na vijana katika kuonyesha vipaji vyao mbalimbali.

Bi. Jaffer amesema maonyesho hayo yanaitwa (MO KIDS GOT TALENT) kwa sababu mdhamini mkuu ni Metl na watakuwa tayari kufanya kazi bega kwa began a watoto, vijana na wazazi wao katika kutambua, kuendeleza na kukuza vipaji vya watoto kupitia maonyesho haya.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Wissem Souifi, amesema maonyesho hayo ni jukwaa pekee kwa vijana na watoto wa Tanzania kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika elimu na Nyanja nyingine za kuburudisha.

“Maonyesho haya yatawajenga vijana kuwa na ujasiri na kuzalisha watu wenye mafanikio mbalimbali katika maisha na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele,” amesema.

Amesema kuwa katika maonyesho hayo wazazi wanaombwa kuwaruhusu watoto wao waende kwenye tamasha hilo kubwa na la kipekee kuandaliwa na makapuni makubwa hapa nchini.
IMG_9722
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi, akihamasisha wazazi nchini kuruhusu watoto wao wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 25, 26 na 27 mwezi Desemba ambapo watoto 100 wa kwanza kujisajili wataingia bure.
DSC_0034
Kisura na Balozi wa MO Beauty Soap Jokate Mwegelo akielezea umuhimu wa tamasha hilo kubwa la Elimu kwa Vijana na manufaa ya kusaka vipaji kwenye umri mdogo ambapo pia amewataka wazazi kuwapa ushirikiano wa kukuza vipaji vya watoto wao.
DSC_0004
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
DSC_0064
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer kwenye picha ya pamoja na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi pamoja na Kisura na Balozi wa MO Beauty Soap Jokate Mwegelo.
DSC_0076
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali, Irfaan Jaffer kutoka MeTL Group pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Fros Africa, Bw. Peter Sekasiko.
DSC_0080
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi akimtembeza Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer maeneo mbalimbali ya hoteli hiyo.

No comments:

Post a Comment