Friday, November 22, 2013

European Film Festival 2013, bonanza la filamu mwishoni mwa wiki



Tamasha la Filamu za Ulaya mwaka 2013 litaanza rasmi Ijumaa tarehe 22 kwa kuonyesha filamu "Untouchables", kutoka Ufaransa katika ukumbi wa Alliance Française saa mbili kamili usiku.
"Untouchables," filamu iliyofanya vizuri kwa mauzo, iliyotayarishwa mwaka 2011, imewekwa katika mandhari ya Paris na inahusu mabadiliko katika maisha ya msomi kutoka familia inayoheshimika, pindi maisha yake yanapokutana na maisha ya Muafrika, ambaye amemfata ili kumwekea sahihi katika nyaraka yake ya uhifadhi wa jamii (social security) ili aweze kupata mafao yake.
Filamu hii imekuwa ikielezewa kuwa ni filamu iliyochangamka, yenye kutia moyo na yenye mguso katika masuala ya ulemavu na rangi lakini muhimu zaidi, ni filamu kuhusu urafiki.
"Tuna furaha sana kuwaletea filamu hii nzuri katika ufunguzi kwa kupitia Tamasha la Filamu za Ulaya ambayo, ingawa ina muonekano mwepesi, ni filamu inayoangalia hali halisi ya ulemavu na urafiki wa watu wasiolingana," alisema Balozi wa Umoja wa Ulaya Filiberto Ceriani Sebregondi.
Filamu 18 zitaonyeshwa mwaka huu katika kumbi nne, Century Cinemax - Mlimani City , Nafasi Art Space, Goethe - Institut na Alliance Française – zote bila kiingilio.
Tamasha la Filamu za Ulaya lilianzishwa ili kukuza uelewa wa utamaduni kati ya Ulaya na nchi washirika wake. Kuna matamasha mengi ya filamu za Ulaya duniani kote na jijini Dar es Salaam tamasha hili limekuwa likifanyika kila mwaka tangu mwaka 1990.
"Ulimwengu unazidi kuwa sehemu ndogo sana lakini bado tunashikilia utambulisho wetu wa kiutamaduni. Filamu ni njia nzuri ya kuonyesha jinsi jamii zinavyoishi kwa namna tofauti na wanavyoshirikiana lakini pia kuonyesha jinsi gani wanafanana. Tuna furaha kuwaletea watanzania na wageni wanaoishi Dar es Salaam filamu za kusisimua bila kiingilio mwishoni mwa wiki hii na tunatarajia mahudhurio mazuri,'' alisema Balozi Sebregondi.
Mwaka huu, tamasha linahusisha maigizo, vichekesho, makala na uhuishaji (animation). Filamu zitakazoonyeshwa mwishoni mwa wiki kuanzia tarehe 22 mpaka 24 zitakuwa kwa ajili ya watu wazima na watoto kwa pamoja.
Baadhi ya filamu zilizochaguliwa zinagusa moja kwa moja tamaduni za Kiafrika, kama vile The Captain of Nakara, iliyodhaminiwa na Umoja wa Ulaya, na The Marshal of Finland kutoka Finland. Nyingine zinatoa mwanga juu ya mifumo ya maisha ya Ulaya kwa wahamiaji au familia za vizazi vya pili.

Nchi zinazoshiriki ni pamoja na Ireland, Ufaransa, Italia, Uswisi, Slovakia, Norway, Hispania, Uholanzi, Ubelgiji , Jamhuri ya Czech , Uingereza, Ujerumani, Denmark, Sweden na Finland. Ujumbe wa Umoja wa Ulaya pia huchangia filamu.
  
Kwa maelezo zaidi wasiliana na waratibu wa Tamasha la Filamu:
Bi Lucian Schim van der Loeff 0652803306 na Bi Kulthum Issa 0767954679

Kwa ratiba na habari kuhusu filamu tembelea:
http://efftanzania.wordpress.com/

http://Facebook.com/efftanzania

No comments:

Post a Comment